Tuesday, October 7, 2014

NYANDA ZA JUU KUSINI - TOUR TO ICE FM RADIO 99.3 (MAY-2014).

Moja kati ya vitu navyopenda katika maisha yangu ni kusafiri , haijalishi kwa Bus, Meli, Ndege, Treni (Japo sijawahi panda), Pikipiki ama Baiskeli....... ili mradi safari... Na-enjoy sana kusafiri maana najifunza mambo mengi na kujua mambo mengi......  Hivyo Mwezi May mwishoni nilipata Tour ya kutembelea sehemu kadhaa za mikoa ya Nyanda za juu kusini, ikiwamo Iringa, Njombe na Mbeya.... Lakini safari yangu ililenga kutembelea kituo changu kipya cha kazi. Nazungumzia Ice Fm Radio 99.3 ya mjini Makambako........ Na safari ilikua kama ifuatavyoNikiwa ndani ya Bus ya JM inayofanya safari zake kati ya Mbeya na Dar...... 

That was an Adventure kutazama miti, misitu, milima, mabonde na Mbuga zetu nzuri na zinazovutia  
(Mikumi National Park).......

Tanzania ni moja ya nchi yenye UTAJIRI wa Rasilimali nyingi sana .... Tazama miti na mabonde yanavyovutia..... 
I'M PROUD OF MY COUNTRY .. I LOVE YOU TANZANIA.

                               
Napenda kushirikiana na kila mtu kwa kubadilishana mawazo na pia ku-share changamoto zinazokabili jamii yetu hasa sisi vijana,,... Huyu ni mchuuzi wa miwa niliyekutana nae mkoani Mbeya wilaya ya Mbalali , Rujewa!!! Asante pia kwa ushirikiano wako maana nilijifunza mengi kutoka kwake!!.


Kwa wasafiri na watumiaji wa Barabara ya Mbeya mtakua mnajua hiki kibao kinapatikana wapi???? Hapa Igawa Junction ya Mbeya na Wilaya Rujewa.......... Lakini pia picha ya chini inaonyesha miundombinu ya Barabara yetu ya kuelekea Mbeya!

Kama lilivyo jina ICE... Likimanisha Information, Communication and Entertainment... So shughuli kubwa za Ice Fm Radio ni kuhabarisha na pia kuburudisha..... hivyoooo ulikua msimu mzuri maana Ice Fm Radio wakishirikiana na Dar Morden Taarabu walikua wameandaa show mbili katika mji wa Makambako na Rujewa Mbeya!!!! 

McDonald Mollel Masse (Kulia) Mkurugenzi wa Ice Fm Radio akipewa utambulisho kwa crowd iliyokuwepo ukumbini na Meneja Masoko wa Ice Fm Bw. Abubakari Aziz....... 


Hapa ni baadhi ya wanamuziki wa bendi Dar Modern Taarabu wakiomngozwa na Hammer Q, pamoja na Meneja wa Bendi Hiyo Bw. Beka wakiwa na Wadau na mashabiki waki-show Love baada ya Show!

Meneja Masoko wa Ice Fm Radio Bw. Abubakari Aziz kibadilishana mawasiliano na Hammer Q mwimbaji maarufu wa Dar Modern Taarab baada ya kuwapagawaisha mashabiki..

McDonald Mollel Masse Mkurugenzi wa Ice Fm Radio akiwa katika shughuli za kuwatambulisha wafanyakazi wake...


Baridi la Makambako sio la kulala mlango wazi.... lazima ujipange sana na majacket na vitu kama hvyo!!! Hapo niki-show Love na Hammer Q baada ya kuwaburudisha mashabiki wake katika ukumbi wa Midtown - Makambako. 

Hapa ni Mwanahawa Ally akiongoza kundi zima la Dar Modern Taarab kuwaburudisha wakazi wa Makambako katika ukumbi wa Midtown.

Mmoja kati ya Best Dj's in Town anafahamika kama Dj Brown a.k.a Dj Mabusuuuu pia ni Head of Entertainment wa Ice Fm Radio......!!! Moja ya kazi kubwaaaaaaaaaaa ni kuwapa watu burudani kama inavyonyesha hapo chini.... mashabiki na wakazi wa Makambako wakiburudika kwa ngoma kali za Taarab kutoka Dar Modern Taarab!!!......

No comments:

Post a Comment