Tuesday, April 15, 2014

R.I.P LEGEND MUHIDIN M. GURUMO.(1940 - 2014)


Sikumfahamu sana kipindi cha utoto wangu simply sikua mpenzi wa dansi mpk miaka ya 2000 niliposikia wimbo wenye kiitikio cha "kuna watu wana roho...... kwa mali alizohacha baba..."  hapo ndio ukawa mwanzo wa kumfatilia mzee mzima Gurumo mpk siku za mwisho za uhai wake.......
 Masaki-kisarawe mkoani Pwani ndipo alipozaliwa mwaka 1940 na pia ndio sehemu alipo pumzishwa katika nyumba yake ya milele leo 15.04.2014 huku mamia ya watanzania wakiongonzwa na makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mh. Garib Bilal waliudhuria mazishi yake. .......
Mwaka 1956 alitinga rasmi Town (dsm) ilala mtaa wa Lindi na mnamo mwaka 1967 safari rasmi ya Muziki ilianza huku akijiunga na Bendi ya Nuta kabla haijabadilishwa jina na kuitwa Juwata na baadaye OTTU JAZZ!!!
 
Japo miaka ya 70 na 80 alipata kuhamia bendi tofauti tofauti kama vile Mlimani Park Orchestra na ile ya Orchestra Safari Sound (OSS - Ndekule) Lakini siku zote maisha yake yamekua Msondo zamani Nuta, Juwata na Ottu Jazz.....! 

Kamanda Gurumo milele atasifika kwa uhodari wake kwani ndiye aliyeifanya Bendi ya Msondo a.k.a Msondo Ngoma Baba ya Muziki Tanzania kupata Heshima kubwa sana hapa Tanzania na nje ya nchi. Siku zote nimepata kusikiliza Tungo zake nimegundua ni Lulu ambayo haitafutika kamwe.......

Kamanda Muhidin M. Gurumo anakuombea raha ya milele na upumzike kwa Amani amina!!!!!!!!!!!!!!.... Wewe umetangulia na sisi tunyuma yako.... salamu kwa Familia ya Msondo iliyotangulia hasa mzee TX Moshi William na Suleiman Mbwembwe.,Bila kuwasahau Albert Mangwear, Langa, Faza Nelly, Complex, Steve 2k, Bi Kidude, James Dandu, Remmy Ongala , Sharo Milionare na wanamuziki wengine waliotangulia mbele ya haki.............!!!