Saturday, November 2, 2013

HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA SAFARI YA MWISHO YA "UNCLE J" PALE VIWANJA VYA LEADERS

 Hapa ndipo mwili wa Marehemu ulipokuwa umeifadhiwa tayari kwa kupewa heshima ya mwisho na kuagwa pale viwanja vya leaders na kusafirishwa kwenda nyumbani kwao musoma kwa ajili ya maziko ...........

 Umati kubwa ulijitokeza kujumuika kwa pamoja ili kutoa heshima ya mwisho na kumuaga nguli wa tasnia ya Habari nchini Julias Nyaisanga "Uncle J" ....... Ukiongozwa na Makamu wa Rais Dr. Bilal, huku wakiwepo wanasiasa, wanahabari na watu mashuhuri nchini kama mwenyekiti wa chadema, Freeman Mbowe na Mkurugenzi mtendaji wa IPP, Dr. Regnald Mengi...............


 Hapa Dr. Regnald Mengi akiwapa pole wafiwa mara baada ya kuwasili viwanja vya leaders.........


 Baada ya msafara toka white house kufika viwanja vya leaders, Dr Bilal alipokelewa tayari kwa kuongoza maelfu ya watu waliokuja kumuaga Uncle J...........!!!!


 Familia, ndugu, jamaa na marafiki walifika kutoa heshima ya mwisho , huku wanahabari hawakua nyuma kuchukua kila tukio lililojili.......

 Mwenyekiti wa Chadema na kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni Mh. Freeman Mbowe baada ya kutoa heshima ya mwisho kwa marehemu Uncle J... alipita pia kuwapa pole wafiwa (Mjane ,watoto na ndg wa karibu wa Uncle J.)........................

 R.I.P Uncle J...... nitakukumbuka kwa mengi sana........ Mungu akupumzishe mahali pema peponi Amina!!! 
Julias Nyaisanga ameacha mjane na watoto watatu.........


 Ni Msiba ulionikutanisha na watangazaji/wanahabari wenzangu karibia wote naowajua na kuwasikia ambao hata sijawahi pata nafasi ya kukutana nao........ Legendary wangu..... napenda kumuita Larry King wa bongo mzee Alfred Masako tukijadiliana kitu na kuchukua ushauri wa hapa na pale...... 

...................."Kutoka eneo la tukio ni mimi Robert Latonga wa Mlimani Tv Elimu Kwanza".................. Ndio maneno niliyosikia hapo kipindi nachukua hii picha... so nimenukuu.....!!!!!