Tuesday, September 17, 2013

WAANDAAJI WA TUZO ZA JAMII NA WADAU KUTEMBELEA KITUO CHA WATOTO YATIMA J'MOSI HII.


Kamati ya maandalizi ya Tuzo za Jamii ikishirikiana na wadau mbalimbali watatembelea kituo cha watoto Yatima j'mosi hii (21.09.2013) kilichopo mtaa wa Yemeni -Tandale kwa tumbo, kiitwacho AL-MADINA CHILDREN HOME .

Kwa mujibu wa mlezi wa kituo hiki Bi. Kurusumu Y. Juma anasema kituo kina zaidi ya watoto 70 ambao wanaishi pale kituoni.
Na mratibu wa tukio ili Bw. ALPHONCE P. MUYINGA (Alphanga Black) ambaye pia ni muasisi na muanzilishi wa Tuzo za Jamii, anawaomba watanzania wote mtakaoguswa kwa namna moja au nyingine kujiunga nao kwa kupeleka misaada kwa watoto wenye mahitaji. Kutoa ni moyo hivyo tujitokeze kuwasaidia watoto/wadogo zetu!!!!

No comments:

Post a Comment