Saturday, September 7, 2013

AZMA WA TAMADUNI MUZIK AFUNGUKA YAKE YA MOYONI KUPITIA NGOMA YAKE MPYA...... "WANASUBIRI NIFE"


Huu wimbo nimeuandika mahsusi kwa ajili ya wasanii na watu ambao wanafanya mambo makubwa,lakini wanapewa sapoti ndogo na kujikuta wanaishi katika maisha magumu ambayo hawa stahili kuishi,kwa sababu tuu watu fulani wameshikilia sanaa yao, na wameamua kuwafanya hawana thamani,ni dedication kwa wasanii ambao hawapewi sapoti na wale wanaopewa sapoti sasa, wasijasahau kwani nafasi walizo nazo kuna wengi walikuwa nazo tena sawa au zaidi yao lakini hawanazo tena.


Kwenye wimbo huu sijamlenga mtu fulani au kituo fulani cha redio/television ila nimewalenga watu ambao wanachangia kukwamisha maendeleo ya sanaa yangu na ya wasanii wengine,haijalishi wako wapi? mfano (Ninaamini mwaka jana wimbo wangu wa Kipimo cha penzi niliomshirikisha Kita ulikuwa ni mmoja wa wimbo bora kabisa kwa mwaka mzima,lakini kuna watu wamejitahidi kuzuia sana usionekane chochote), ni watu wachache tuu wanao amua iwe hivi, tena kwa sababu zinazojulikana moja wapo alishaisema kaka mkubwa Fareed Kubanda katika kibao chake cha proganda "wadau wana wasanii wabovu, je wakali mtasikika vipi? "

Na haya ni baadhi ya makundi ambayo ningependa huu wimbo uyafikie:


1. SERIKALI
Serikali inahusika kwa asilimia zaidi ya tisini na tano kuchangia uwepo wa tatizo hili, kwani haijatengeneza mifumo bora kwenye sanaa, na haijaichukulia sanaa kama chanzo cha Ajira, hivyo kusababisha,wenye pesa wanaendelea kuwaibia wasio na pesa kwa sababu soko ni huru.


2.VYOMBO VYA HABARI
Nazungumzia redio, television,magazeti nk,Vyombo hivi vina mchango mkubwa sana katika kuifikishia jamii taarifa,Baadhi ya watendaji/wamiliki wa vyombo vya habari wanavitumia vyombo vyao kudidimiza maendeleo ya sanaa kwa baadhi ya wasanii na kuwainua wachache, vyomba vya habari pia vinawagawa wasanii pasipo sababu ya msingi, mfano mziki wa hip hop ,reggae nk hausapotiwi.


3. MASHABIKI/JAMII KWA UJUMLA.
Wasanii wanafanya kazi si kwa ajili yao tuu, lakini wanafanya  kwa sababu ya jamii, jamii inapaswa kuwaunga mkono ili kuboresha maisha yao,ila hali imekuwa tofauti nchini, jamii haitoi sapoti inavyotakiwa, hii leo mtu yuko radhi aendelee kuyatajirisha makampuni ya simu ya wahindi kwa kununua bandle za maelfu kumi matatu ,manne au hata matano ili apate kifurushi cha kudownload/kupakuwa kazi za wasanii bure, lakini akawa hayuko tayari kununua album ya msanii kwa shs 5000/=tuu.


4. WASANII NA WATAYARISHAJI
Wasanii wengi ni wanafiki hasa wale wasio na uwezo, watu tunarogana watu wanapandikiza chuki kwa wasanii wengine, hasa wakiona kitu kizuri wanajifanya wanakandia,kwa sababu wao wanajua hawawezi kufanya hivyo,halafu likitokea suala la msanii amefariki, utawasikia jamaa alikuwa noma sana yule,ndio maana hii leo msaanii yuko tayari kupokea tuzo ya reggae au Hi hop wakati yeye hafanyi mziki wa aina hiyo,huku akimuona msanii anayefanya mziki huo akiikosa huku akiwa huru na kujitapa yeye anaweza,hii leo wasanii ambao ni waigizaji kabisa wanakosa ajira kwa sababu ma modal ma beautifully au ma handsome wamaevamia soko la filamu,siku hizi filamu na video za wasanii zinauzwa si kwa sababu zina waigizaji wazuri, ilatuu  kwa sababu wameweka watu ambaye ni mzuri wa umbo au sura au ni  maarufu.


MATARAJIO YANGU
Ningependa Wasanii tujifunze kwa yaliyotokea kwa wasanii wenzetu kama Sajuki,Kanumba, Sharo milionea, Langa na Alberrt Mangwea,baadhiyao,wamefariki wakiwa na umaarufu mkubwa kwa jamii, mfano: karibu kila nyumba ya Tanzania ilikuwa na filamu ya Kanumba au ya Sajuki lakini je wao wamekufa wakiwa na nini?,je mafanikio ya msanii ni nyumba na gari? na Mangwea alikuwa akionekana si chochote kwenye sanaa yake siku za mwisho wa uhai wake na baadhi ya watu wakawa wanadai jamii imemchoka yeye na mziki wake, lakini siku ya msiba wake ilikuwaje? walipokuwa wakicheza nyimbo zake siku ya msiba tumejifunza nini?

 
NINA MENGI SANA....siwezi kuyamaliza ila naomba WATANZANIA tubadirike  TUWE NA HOFU YA MUNGU NA TUHESHIMU KINACHOFANYWA NA WENGINE, HATA KIDOGO TUU NA TUMAANISHE KWA HILI.

NB
Naomba msanii/mwanajamii/mtu yeyote ambaye unaguswa na hili suala  la watu KUSUBIRI TUFE ILI WAONE UMUHIMU WETU,apate kushare  huu wimbo kwa  Watanzania wengi iwezekanavyo, ikiwa kama hatua moja ya kuonyesha hisia yetu,Watu wa blogs, magazeti nk hili linawahusu pia....


WIMBO: WANASUBIRI NIFE
ARTIST: AZMA (EI ZED EM EI)
PRODUCER: DOUBLE
STUDIO: GLORY RECORDS /DODOMA
SIMU:0712738888 - Endapo mtu una hitaji kuniunga mkono kunua ALBUM YANGU (LOVE STORIES)

VITENDO DHIDI YA MANENO.

No comments:

Post a Comment