Sunday, September 22, 2013

HAPPINESS WATIMANYWA NDIYE MISS REDDS TANZANIA 2013Mrembo Happiness Watimanywa (19) ambaye pia ni Miss Dodoma 2013, Miss Kanda ya Kati 2013 na Redds Miss Photogenic 2013 ndiye kashinda na kuvishwa taji la urembo la Redds Miss Tanzania 2013. 


Huku akiondoka na zawadi ya gari aina ya Toyota IST , na kitita cha fedha taslimu za kitanzania shilingi Milioni 8. Huku tukitegemea kwenda kutuwakilisha katika mashindano ya dunia yanayotegemewa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu !!!

Tunampongeza Happiness Watimanywa, na Hongera watu wangu wa Dodoma !

WASANII NA WAANDAAJI WA TUZO ZA JAMII WATEMBELEA KITUO CHA WATOTO YATIMA (Al-Madina Children Home).

 Kamati ya maandalizi ya Tuzo za Jamii leo wamejumuika na wasanii wakongwe wa mzuki wa kizazi kipya ,pamoja na wadau wengine kutembelea kituo cha watoto Yatima kilichopo maeneo ya Tandale kwa tumbo kiitwacho Al - Madina Children Home. Ikiwa ni ishara ya upendo na pia kushiriki pamoja na watoto hao kwa namna moja au nyingine...... Wakiongozwa na Prof. Jay, the Heavy Weight Mc a.k.a Dady a.k.a Mr. Red Carpet a.k.a majina mengi kutoka Choka mbaya , pia alikuepo Black Rhino na Saprano!!! Pia na wadau wengine waliwakilisha kwa sana!!! Yafuatayo ni matukio ktk picha kwa yale yaliyotokea!!! Haya twende sawa:-

 Show timeeeeeeeeeeeee....... Black Rhino, Prof Jay , Alphanga black wakishow lov!!
 Kama kawa , kama dawa nilijumuika kushow lov , Arnie G, Rhino, Saprano, Jay na Mh. Masanga

 Palipo na wengi hapakosi jambo..... Salute sana kwa kaka mkubwa Prof. Jay zaidi ya muziki pia ana kipaji kikubwa sana cha uchekeshaji.... So i believe hasingekua Mwanamuziki basi tungekutana naye kwenye Comedy ....... ukiwa na Prof Jay lazima ucheke.... daaaah!!!!

 Baada ya kufika eneo la Tukio tukaanza kupakua Gift za hapa na pale tulizowaletea wadogo/watoto wetu kwa upendo kushare nao kwa namna moja au nyingine!!!!


 Hawa ni baadhi ya watoto waliotupokea hapo nje!! hawakusita kuonyesha hisia zao kwa Prof jizzee ......

 Tukakaribishwa ndani kwa utambulisho wa hapa na pale, pia tukapata nasafi ya kuongea na mlezi wa kituo Bi. Kurusumu Juma ambaye alitupokea kwa upendo na pia kutupatia Historia fupi ya kituo hicho!!!

 Ni kituo chenye Takribani watoto 70 na chenye changamoto nyingi, lakini kuna changamoto ambazo ni sugu kama suala la Karo za watoto shule ,bill za umeme na maji pamoja na suala la matibabu .(kwa mujibu wa Mama mlezi wa kituo hiki). Hivyo tunaomba wadau kujitokeza kwa ajili ya misaada zaidi ili watoto hawa wapate Huduma zote muhimu. (Elimu, Afya na Mahitaji yote muhimu)......!!


 Kutoka kushoto ni Saprano, Arnie Gizzle, Black Rhino, Bi. Kurusumu na Prof. Jay kwa makini tukimsikiliza Alphanga Black (ambaye hayupo pichani) akielezea kwa kifupi ujuo wetu na Kuguswa na watoto hao.

 Ikafika muda wa kuongea na wahusika , ambao ni watoto wa kituo hicho cha Al-Madina Children Home, kitu kilichonifurahisha sana ni pale kila mmoja alikua na shauku ya kumuona Prof. Jay!!!!


 Haya watoto wote kidole kimoja juuuuuuuuuuuuuuuuu kuonyesha ishara ya upendo!!


 Kitu cha muhimu sana kutoka kituo hiki ni kwamba watoto wote wanalelewa katika maadili ya dini , hvyo kila kitu kwao umtanguliza Mwenyezi Mungu mbele!!! ...... Baada ya kushare story za hapa na pale na watoto, tukapata nafasi ya kipekee kwa ajili ya kuombewa dua!! kila mtu aliweka viatu vyake kando na kuingia ndani kupata baraka kupitia sala za watoto !!!!!
 Haya baada ya Dua tukapata nafasi ya kuagana na Bi. Kurusumu ambaye ni mlezi na mmiliki wa kituo, na pia tukaitumia nafasi hiyo kwa kuongea nae mawili matatu na kumuahidi kuwa tutajitahidi kushirikiana na wadau wengine kuendelea kuja na kushare chochote tutakacho kipata!!!!!


 Tukapata muda pia kuwasikiliza watoto malengo yao ya  baadae na pia ndoto zao ni nini wakiwa wakubwa!!! Huo ulikua pia muda mzuri sana kwao na kwetu, ( Swali zuri kutoka kwa Black Rhino)!!!!

 Anafahamika kama Saimon 18, ambaye ni C.E.O wa Hot Spot Magazine ( Hotspotmagazine.co ) akishow lov na mtoto ambae ndio mdogo pale kituoni, mtoto huyo anafahamika kwa jina la Ridhiwan.
 So ikafika wakati wa Prof Jizzeeeee kushusha mistari kwa watoto..... ha ha ha ha h a msanii uingie kwa mtu ubanduke bila swaga !!! wacha bhana!!! "..... haya twende kindergarten hadi chuo kikuu............ masister duuuuu...... hapo vipi,......?" ni moja ya mistari ya Jay kwa watoto.... nao hawakusita kusema HAPO SAWAAAAA!!!!! 
 Mwisho wa siku tukashow Love kwa kunyosha kidole kimoja juuu bila kujali itikadi yoyote kwa manufaa ya watanzania wote!!!! 

Zaidi niwashukuru wote kwa kushiriki tukio . Sana nimpe pongezi za dhati muasisi wa Tuzo za Jamii Bw. ALPHONCE a.k.a Alphanga black kwa mawazo yake endelevu pia kwa kujali sn jamiii ya mtaa zaidi na kutuunganisha pamoja kujumuika kwa tukio ili muhimu.

Shukrani zangu pia ziende kwa Wasanii kama Prof. Jay ambaye kahacha kazi zake na kujumuika nasi, pia mdogo wake Black Rhino akiwa na mshikaji wake Saprno kwa kuonyesha moyo na ushirki wa hali ya juu kwa tukio hili...

Pia kwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Ccm wilaya ya kinondoni Bw. Said Masanga bila kujali itikadi za vyama kajali sana utu wa watoto hawa na kuhacha shughuli zake na kuja kujumuika nasi........!!!

Sitakua nimetenda haki kama nisipomshukuru my Lovely wifey kwa Support yke , kwani alikua mwanamke pekee kati ya wote tuliojumuika kushiriki kwenye ili tukio.....She always there 4 me!! Thnx so much!!!!


NIPENDE TU KUWAOMBA SANA WATANZANIA WENZANGU KUWA NA MOYO WA KUSHIRIKI MAMBO YA KIJAMII KAMA HAYA BILA KUJALI WEWE NI NANI NA UNA NINI. HATA KITENDO CHA KUWAFIKIA WATU WENYE HUITAJI KINATOSHA KUWAFARIJI!!!!