Saturday, August 31, 2013

PROF. JAY, ZEMBWELA (East Africa Radio) NA ADAM MCHOVU (Clouds Fm) WAPATA TUZO ZA HESHIMA ZA JAMII.

 Nilipata nafasi ya kukabidhi Tuzo kwa mmoja ya washindi wa Tuzo za Jamii, Tukio ilo la makabidhiano lilifanyika ktk Ukumbi wa Melmoz ulipo kawe jirani na viwanja vya Golf Lugalo. Pia iliudhuliwa na watu mbali mbali wakiwemo wanasiasa , wanamichezo ,wasanii na watu wa kada tofauti tofauti.

Prof. Jay alikua miangoni mwa watu waliopata Tuzo hizo za Heshima kutoka kwa jamii kutokana na mchango wake ktk jamii, na wengine walikua ni pamoja na mtangazaji wa East Africa Radio kupitia kipindi cha Super Mix Zembwela na Mtangazaji wa Clouds Fm Adam Mchomvu.

 Kwa niaba ya Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Ccm (UVCCM) wilaya ya kinondoni nilipata nafasi ya kukabidhi Tuzo kwa mwakilishi wa Adam Mchomvu wa Clouds Fm.
 
 Kama mfanyakazi na mwakilishi wa Adam Mchomvu, alipata nafasi ya kuelezea furaha yake kuhusiana na kupata Tuzo ya Heshima kutoka kwa jamii...

 Hapa tukapata kupiga picha ya pamoja ku-show some love na respect kwa waandaaji wa Tuzo hizo!!

 Ni moja ya wafanyakazi wa East Africa Radio na pia ndio alikuwa mwakilisha wa Zembwela, ambaye akufika kutokana na majukumu mengine ya kikazi . Hapa akionyesha furaha yake baada ya kukabidhiwa Tuzo.

 Hapa ni Prof. Jay, The heavy weight Mc, Mr. Red Carpet au Jay wa Mitulinga akifanya mahojiano na Waandishi wa Habari kuelezea Furaha yke na heshima aliyopata kutoka kwa jamii baada ya kukabidhiwa Tuzo yke!!!

 Baada ya Mahojiano alifanya kupata picha ya Pamoja na Robert Latonga , mwandishi wa Habari na mwanaharakati kutoka Mlimani Tv ya chuo kikuu cha Dsm (Udsm). Huku akionyesha Tuzo hyo aliyochongwa kwa malighafi ya mti wenye thamni sana Duniani , na ambao hupatikana kwa wingi Tanzania. Mti aina ya Mpingo.

 Furaha kubwa ni pale Prof. Jay alipokutana na DJ JD (John Dilinga) The EverLasting Dj na kushow some Love with  the Respect kwani ni mmoja kati ya wadau walioufikisha muziki wa Bongo Fleva hapa ulipo. Pia inasemekana jina la Prof. alimetungwa na Dj JD mwenyewe !!!!

Kutoka kushoto ni Salum, Prof. Jay, Allan Lucky (East Africa Tv) ,Alphanga Black na jamaa wakishow some love na Furaha yao kwa kumpongeza Prof. Jay baada ya kukabidhiwa Tuzo ya Heshima kutoka kwa jamii kama Msanii Mwenye mchango mkubwa kwa Jamii.

 Hapa Dj JD alipata fursa ya kuongea na wanahabari kuelezea machache kuhusu Muziki wetu ulipotoka ,ulipo na unapoelekea. Pia akiwasihi wadau kutoa Support kwa waandaaji wa Tuzo hizi.!

 Tulipata kupiga picha ya pamoja na waandaji wa Tuzo na waliotunikiwa kama kumbukumbu kwa tukio muhimu .
 Ni moja kati ya wageni waalikwa katika Tukio la ugawaji wa Tuzo za Jamii... Kushoto ni Bw. Masanga ambaye ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Ccm (UVCCM) wilaya ya Kinondoni akiwa kwenye picha ya Pamoja na Dr. Nassoro Ambaye pia ni Mwenyekiti wa Madaktari wa Michezo Tanzania.

 Nikapata pia Nafasi ya Kupiga picha ya pamoja na Dj JD, Dr. Nassoro na Alphanga Black ambaye ndio mwanzilishi wa Tuzo hizo za jamii, hii ni  muda mfupi baada ya kubadilishana mawazo ya namna gani tunaweza kuziboresha!!!!

 Anafaamika kama Alphonce lakini wengi tunamjua kwa jina la Alphanga Black... huyu ndie Founder wa Tuzo za jamii na pia ni mmoja kati ya waandaaji wa Tuzo hizo..... hapa akihojiana na wanahabari kuelezea mafanikio na changamoto anazokutana nazo ktk mchakato mzima wa uandaaji wa Tuzo hizo!!!

Kutoka Kushoto ni Bw. Salum ambaye pia ni mmoja ya waandaji wa Tuzo za Jamii, DJ JD, Arnie Gizzle na Dr. Nassoro .

Kwa mtazamo wa wengi hizi ni moja kati ya Tuzo ambazo zinatazamiwa kuwa Tuzo kubwa kwa ukanda wa Afrika Mashariki na kati kama zitapata Support ya kutosha kutoka kwa wadua na jamii kwa ujumla bila kusahau support ya Serikali hasa wizara husika na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA).

Nipende kutoa pongezi kubwa kwa waandaji wote wa Tuzo na pia kwa wageni wote mliofika bila kujali changamoto za foleni za Dar.... na pia natoa wito kwa Makampuni makubwa kumsuport Alphonce na waandaaji wa Tuzo hizi.

No comments:

Post a Comment