Friday, August 9, 2013

BAADA YA Ft. NA FID Q KWENYE NGOMA YA SIHITAJI MARAFIKI, MZAMBIA YVONNE MWALE AJA NA NGOMA MPYA YA "ACHA UMBEA"
Sio muda sana toka Msanii wa Afro-Jazz  Yvonne Mwale ame-launch album yke ya 'Kalamatila' in Dar es Salaam na kuteka umati mkubwa wa fans alionao hapa Tanzania. Kama mzaliwa wa Zambia na msanii ambaye amepiga tour zaidi ya Nchi 8 Europe mwaka 2010 na baada ya hapo akaamua ku-settle Tanzania kuendeleza kazi zake za music. Matokeo ya Albam yake ya pili ya 'Kalamatila' ndio yalimpatia nafasi ya kujulikana kama solo artist, na hii ni kupitia single na video yake ambayo ilipata Airtime ya kutosha kwa vituo mbalimbali vya Tv hapa Africa Mashariki..... Ngoma iliyokwenda kwa jina la 'Familia Yangu'.

Umaarufu wake umekua zaid baada ya ku-release collaboration na Mkali wa Hip Hop Tanzania Bw. Farid Kubanda Known as Fid Q, kwenye mkwaju mkali sana uliokubalika na kuwa Super-Hit all over East Africa.......... Ngoma iliyokwenda kwa jina la 'Sihitaji Marafiki' .... Ambayo kwa muda mchache tu ikawa inaongoza kwenye Charts mbalimbali za radio na TV kwa week kadhaa. Mwishowe, the same song was nominated kwenye category mbili tofauti za Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013.

Kama Asante kwa Fans wake wote wa East Africa na Ma-supporter wakubwa... Basi Yvonne kaamua kushusha ngoma mpyaaaaa ambayo imeandikwa kiswahili kama zawadi kwenu bureeee kabisa. The Song goes by the name of 'Acha Umbea' kama vipi fanya kubofya hapa ili kuisikiliza na pia kuipata: http://www.reverbnation.com/yvonnemwale/song/18188029-acha-umbea

Right now Yvonne karudi  Europe ambapo ataanza Tour fupi huku akijiandaa ku-Record Albamu yake ya TATU in one of the Major music studios in Germany.


Yvonne Mwale on Facebook: http://www.facebook.com/YvonneMwaleMusic
Yvonne Mwale on YouTube: http://www.youtube.com/yvonnemwale

No comments:

Post a Comment