Sunday, July 1, 2012

WINIFRIDA DOMINIC : MISS UNIVERSE TZ 2012.


 MISS UNIVERSE TZ 2012 ni Winfrida Dominic kutoka Dsm na kunyakuwa mkwanja wa kibongo Mil. 3 na bonge moja la ofa ya kwenda kupiga book unyamwezini katika chuo cha New York Film Academy , zaidi ya hapo pia ataiwakilisha Tanzania katka mashindano ya Dunia hapo baadae.

Huku nafasi ya pili ikienda kwa Bahati Chando nae kutoka Dsm ambaye pia alidaka Mil.1 na kupata nafasi ya kuiwakilisha Tz ktk mashindano ya Miss Earth, huku nafasi ya tatu ikishikwa na Dorice Mollel aliyepata Laki 5 na nafasi ya kuiwakilisha Tz katika mashindano ya Miss Tourism Queen International.


Nafasi tano bora zote zilichukuliwa na warembo kutoka Dar Es Salaam, kitu ambacho kimeonekana kama changamoto kwa warembo wanaotoka mikoani. Compass Communicatin chini ya Maria Sarungi ndio wandaaji wa Mashindano haya kwa miaka kadhaa mfululizo.