Thursday, June 14, 2012

MAKAVULIVE FT. JOSLINE WAMEFUNGUKA KUTOKA BONGO RECORDS.


Baada ya kimya kidogo, Makavulive chama wameachia kitu tena wakiwa wamefanya wasanii watatu Dullayo, Mon-G na Joslin ktk Studio za BONGO RECORDS chini ya Producer mwenye mapinduzi makubwa ktk Bongoflava industry hapa Tanzania.. P FUNK aka "Majani", pia kuna touch za Guitar zilizopigwa na "Mzungu Kichaa".

Ngoma inaitwa FUNGUA, ipo ktk mchakato wa Project ya Makavulive ambayo inatazamiwa kumalizika mwishoni mwa mwaka huu '2012'. so mkao wa kula ndio mpango mzima.

Thursday, June 7, 2012

TANGAZA NASI MSIMU WA SABASABA KUKUZA BIASHARA YAKO.


Kama una Biashara yoyote karibu ktk kijarida chetu cha kila mwaka kinachotoka mara moja kwa mwaka na ktk msimu wa sabasaba. so fanya kutangaza nasi kwa maendeleo ya biashara yako,......"BIASHARA MATANGAZO" Bei zetu ni poa sana.

Kwa mawasiliano zaidi Mob: +255 713 575662

                                                +255 713 528590

                             Email:  arniegizzle@yahoo.com
                                        visualsigns08@gmail.com

JEMBE LA KASKAZINI - BOUNAKO!!!!!!!


Mzee mzima D Double anayejulikana vema zaidi kama BouNako a.k.a Jembe la kaskazini anadondosha dudeee brand new kwa fans wote wa hiphop duniani..hii ndio "Jembe la kaskazini"(download hapa),ikiwa ni single inayofata "Mara Hoo" ambayo imefanya vema mtaa na media kwa miez mitatu ilopita.

"Game ni gumu tangu enzi za baba zetu lakini kukata tamaa sio suluhu wala haisaidii, nakomaa kwa maana mashabiki zangu ndio wananipa nguvu ya kutifua,  hii ni zawadi kwenu kwa support yenu kununua T-shirt za J.E.M.B.E na iko wazi mimi sio kitu bila ninyi, skilizieni more tingz zinakuja "walete" pamoja na "acheni".. ANAFUNGUKA BOUNAKO.

Tuesday, June 5, 2012

BOGA NA UA LAKE - NGOMA MPYA YA C-SIR MADINI

 Baada ya Nishike Mkono iliyotoka January mwaka huu na video yake kutoka April 2012, Now katoa  new release inayokwenda kwa jina la BOGA NA UA LAKE.

Namzungumzia C-SIR MADINI kutoka Rock City chini ya Tetemesha Records huku wimbo huu ukiwa  wenye ujumbe wa moja kwa moja kama ukiuskiliza kwa makini utauelewa. Unahusiana na Kumpenda mtu kama alivyo na mapungufu yake yote. 

Katika wimbo huu C-sir ameimba amempenda binti lakini baadae kaja kugundua kuwa binti ni muathirika wa gonjwa la ukimwi, lakini hiyo haikuwa sababu ya yeye kumuacha na akaendelea kusisitiza pamoja na yote hayo hatamuacha. (Sio story ya kweli ni utunzi tu kuwakilisha yaliyoko mtaani)

CREDITS

ARTIST:  C-SIR MADINI
SONG: BOGA NA UA LAKE
COMPOSER: C-SIR MADINI
PRODUCER: KID BWOY
STUDIO: TETEMESHA RECORDS (DAR)

GENTRIEZ KUTOKA RIVER CAMP SOLDIER.
Gentriez mwakitabu ni msanii wa Hip-Hop kutoka kundi la River Camp Soldiers jijini Arusha. Alianza mziki mwaka 2003 kupitia talent shows na free stage hasa zile za Via-Via. 2008 aliingia studio na kurecordi wimbo wake wa kwanza uliokua unaitwa Mandamano Ya Haki ambao hauku fanikiwa kufanya vizuri..then 2011 hapo ndipo nyota yake kidogo ilipoanza kuonekana baada yakuachia .uliofanya vizuri kuanzia mtaani hadi kwenye radio statiotion tofauti. Pia wimbo huo ulikuja na mafanikio kadhaa kama, alipatiwa jina la Arusha boy pia akafanikiwa kufungua clothing line ya Arusha boy clothing line chini ya Wanene Entertainment.. and now 2012 ameachia wimbo wake mwingine unakwenda kwa jina la  NNA KILA SABABU aliomshirikisha msanii mwingine kutoka kundi la Jambo Squad Chalii Mtoto Wa Bibi au Nigga C.. humo ndani utaskia michano mikali 

Watu wakae tayari kwa ujio wa video ya wimbo huo itakayo toka hivi karibuni.. Pia unaweza kuskiliza na kudownload bure nyimbo kibao zake zote alizowahi kuzifanya  ONLINE kupitia:


 Gentriez mwakitabu mpaka sasa ameshaafanya kazi na wasanii wakubwa kama  NAKAYA,G,NAKO,BONTA,[WEUSI].DEF XTRO[NOIZMEKAH]BELLE 9, NAH REEL, MESEN SELEKTA,JORS BLES,MONA GANGSTA NA WENGINE WENGI..

Gentriez Mwakitabu yuko chini ya RECORD LEBEL YA WANENE ENTERTAINMENT iliko jijini Arusha inayo milikiwa na founder and C.E.O Darsh Pandit.