Saturday, May 19, 2012

KWANINI MEDIA ZINAZIDI KU-PROMOTE BEEF KWA WASANII????


This friday kabla ya kujipanga 4 da wkend nilikuwa home watching Tv... Daaaah hasara kwa Tv fulani hapa Town ambayo......... [sitahitaja Tv kwa kutunza heshima] walikuwa wakifanya Interview na Rais wa Masharobaro Bongo ambaye pia ni prodyuza na msanii wa muziki wa Kizazi Kipya, Raheem Rummy Nanji  a.k.a Bob Junior Swali ambalo sikutegemea ni pale Presenter moja kati ya Presenterz waliokuwa waki-Host show hiyo kuhusiana na kauli ya Diamond siku ya tunzo za KTMA 2012 baada ya Ommy Dimpoz kupata Tunzo.

Baada ya kutangazwa ushindi wa Dimpoz, Diamond alimsindikiza stejini na kutoa kauli kuwa kipindi fulani alimpeleka DIMPOZ kwa Producer mmoja [akimlenga Bob Junior] na jamaa kumtosa na kumtimua Dimpoz kwamba hajui kuimba lakini cha ajabu leo hii  Dimpoz kapata tunzo na huyo Producer hajawahi kupataTunzo kamwe.

 


Japo na jitihada za kutaka kulikwepa swali lakini kama ma-Presenter walikomalia kumuuliza kwa msisitizo mpk Bob J alipofunguka na kusema  "DIAMOND ni mtoto mdogo so analopoka sana bila kuangalia anaongea nini  na anaongea na nani?"
Zaidi Bob J alisema hawezi sema lolote juu ya ilo na kuongeza kwa kusema kitendo cha kumchomolea Dimpoz enzi hizo anaamini ndio kimemsaidi  kufika hapo alipo leo otherwise angebweteka sana zaidi alifanya mazoezi yaliyomwezesha kufika hapa alipo.

Wale Presenterz kama walikuwa wametumwa na mtu fulani kuchochea maswali ya Uchonganishi utazani yana msingi kwani katika namna moja au nyingine Bob J alikuwa anakimbia maswali yao kwa kuwambia "Naomba tusiongelee haya mambo" Jamaa wamo tu utadhani wameambiwa bila kumuliza hayo maswali hawatapata salary ya mwezi huu.
Mwishowe kama kuwakata kilimi Bob J kwa upole sana alisema "kuongelea suala la DIAMOND ni sawa na kupoteza muda wangu kwani Diamond hana faida wala msaada wowote kwangu, kwani kwa sasa sina hata mawasaliano yoyote na hata tukikutana kitaa hatupeani hata Hi!"

HAPO NIKAKUMBUKA NGOMA YA FID Q YA PROPAGANDA KWENYE ILE CHORUS......... Kama hujaisikia ngoma hii fanya kuitafuta na utajua Fid alikuwa anamanisha nini??

MEDIA KUZENI NA KU-PROMOTE VIPAJI NA SIYO KU-PROMOTE BEEF!!!!!!!!!!!!!! HACHENI HIZO BHANA!!!!!!!!!
Zaidi nakupongeza sana BOB JUNIOR kwa majibu yenye busara kwa kuwacholesha makanjanja hawa na pia ni jambo la kuigwa na Wasanii WOTE. na sio kuongea bila mpango kisa upo kama unaongea na washikaji na sio Media.!!!

No comments:

Post a Comment