Saturday, May 19, 2012

BOB MARLEY DAY 2012.


Leo ni siku ya kumbukumbu ya kifo cha Bob Nester Marley so hapa nyumbani Tanzania kwa mwaka wa saba mfululizo tumekua tukimkumbuka kwa namna ya pekee , hivyo basi, kesho kutakua na band 4, ambazo ni Ras Inno,Ras Mizizi,Jhikoman na Worriers kutoka Arusha ambao walitwaa tuzo ya best Reggae band 2012 katika Kilimanjaro Tanzania Music Awards.
kutakua na wasanii wa kizazi kipya cha reggae waitwao Susu man,Jah Son,Dabo,Chibwa,Ras Six hao wa kizazi kipya,ukichanganya band na wasanii wa kizazi kipya cha reggae kutakua na wasanii zaidi ya 55 back stage.

Pia kutakua na ragga dancers, wapenzi wote wa Mpira LEO finaly ya Champions legue kati ya Chelsea na Bayern Munich ambayo itaoneshwa live katika big screens, isseu nzima inaanza saa mbili usiku mpaka majogoo kiingilio ni tshs 5000/=.

ONE LOVE NDIO MSISITIZO WA BOB MARLEY!! 
PEACE & LOVE PALE VIWANJA VYA POSTA KIJITONYAMA ....!!

KWANINI MEDIA ZINAZIDI KU-PROMOTE BEEF KWA WASANII????


This friday kabla ya kujipanga 4 da wkend nilikuwa home watching Tv... Daaaah hasara kwa Tv fulani hapa Town ambayo......... [sitahitaja Tv kwa kutunza heshima] walikuwa wakifanya Interview na Rais wa Masharobaro Bongo ambaye pia ni prodyuza na msanii wa muziki wa Kizazi Kipya, Raheem Rummy Nanji  a.k.a Bob Junior Swali ambalo sikutegemea ni pale Presenter moja kati ya Presenterz waliokuwa waki-Host show hiyo kuhusiana na kauli ya Diamond siku ya tunzo za KTMA 2012 baada ya Ommy Dimpoz kupata Tunzo.

Baada ya kutangazwa ushindi wa Dimpoz, Diamond alimsindikiza stejini na kutoa kauli kuwa kipindi fulani alimpeleka DIMPOZ kwa Producer mmoja [akimlenga Bob Junior] na jamaa kumtosa na kumtimua Dimpoz kwamba hajui kuimba lakini cha ajabu leo hii  Dimpoz kapata tunzo na huyo Producer hajawahi kupataTunzo kamwe.

 


Japo na jitihada za kutaka kulikwepa swali lakini kama ma-Presenter walikomalia kumuuliza kwa msisitizo mpk Bob J alipofunguka na kusema  "DIAMOND ni mtoto mdogo so analopoka sana bila kuangalia anaongea nini  na anaongea na nani?"
Zaidi Bob J alisema hawezi sema lolote juu ya ilo na kuongeza kwa kusema kitendo cha kumchomolea Dimpoz enzi hizo anaamini ndio kimemsaidi  kufika hapo alipo leo otherwise angebweteka sana zaidi alifanya mazoezi yaliyomwezesha kufika hapa alipo.

Wale Presenterz kama walikuwa wametumwa na mtu fulani kuchochea maswali ya Uchonganishi utazani yana msingi kwani katika namna moja au nyingine Bob J alikuwa anakimbia maswali yao kwa kuwambia "Naomba tusiongelee haya mambo" Jamaa wamo tu utadhani wameambiwa bila kumuliza hayo maswali hawatapata salary ya mwezi huu.
Mwishowe kama kuwakata kilimi Bob J kwa upole sana alisema "kuongelea suala la DIAMOND ni sawa na kupoteza muda wangu kwani Diamond hana faida wala msaada wowote kwangu, kwani kwa sasa sina hata mawasaliano yoyote na hata tukikutana kitaa hatupeani hata Hi!"

HAPO NIKAKUMBUKA NGOMA YA FID Q YA PROPAGANDA KWENYE ILE CHORUS......... Kama hujaisikia ngoma hii fanya kuitafuta na utajua Fid alikuwa anamanisha nini??

MEDIA KUZENI NA KU-PROMOTE VIPAJI NA SIYO KU-PROMOTE BEEF!!!!!!!!!!!!!! HACHENI HIZO BHANA!!!!!!!!!
Zaidi nakupongeza sana BOB JUNIOR kwa majibu yenye busara kwa kuwacholesha makanjanja hawa na pia ni jambo la kuigwa na Wasanii WOTE. na sio kuongea bila mpango kisa upo kama unaongea na washikaji na sio Media.!!!

Saturday, May 12, 2012

KUTOKA A -TOWN UNAWAJUA HAWA JAMAA???

Contagious B-Boys a.k.a A-CITY BOYS; Ni Kundi la dancers mahiri from Chuga Town ambao pia ni waimbaji wa Music, Currently wamedrop brand new Ragga Dancehall track ijulikanayo kama "More Than" na hii ni kazi ya kwanza tangu Warudi kutoka Ghana kwenye mashindano ya kudance!
 
 
  Humu ndani katika hii track Wamezungumzia manzi mkali anayesumbua jiji na also wamerecord Audio hii kwa Defxtro Hapa hapa chugatown  Contagious wenye maskani yao pande za Arachuga wamekuwa bize zaidi wakijifua kwa mashairi na sauti kwa ajili ya kumudu Game.

Waburudishaji hawa pia wameahidi kung'ara zaidi katika medani ya kuvunja majoka a.k.a.Breakdancing kwa vile team yao sasa imeongezeka dancers wapya na vile vile mazoezi yanakwenda kiubunifu zaidi,Shukrani milioni nane ziende kwa mafans wao na wadau wote katika Media ndani na nje ya bongo pamoja na dunia nzima!!!

Cheki News zaidi ghana ilivokuwa...

http://www.dailyguideghana.com/?p=21609

http://www.arushatimes.co.tz/2011/26/Local%20News_2.htm

WHO GOT TALENT?


"WHO GOT TALENT?
LOCAL TAILORING & DESIGNER COMPETITION IZ COMING..
Presented to you by EVENTS WORLD...
StaY tUNed..!!!!

MOJA MOJA TRACK MPYA YA DARK MASTER FT. HARDMAD

Track mpya kabisa ya mtu mzima kutoka Chamber Squd Dark Master inayokwenda kwa jina la MOJA MOJA na humo ndani kuna mshindi wa mwaka jana wa KTMA na mkali wa corus HARDMAD....

Lyrics ambazo zimeandikwa na mtu mzima mwenyewe DARK MASTER chini ya Produced TIDDY HOTTER katika Studio za ONE LOVE FX Jijini MWANZA.
Ni ujio mpya wa Dark so mashabiki kaeni tayari kumsoma coz kitambo sana.