Tuesday, March 27, 2012

HIP HOP DANCERS WAPO HIVI.

Ukiizungumzia Hip Hop in General utakutana na mambo mengi hasa zikiwamo nguzo zake nne ambazo ni DISC JOCKEYS {DJ'S}, GRAFFIT {ART}, MC'S {RAPPERS}, na B-BOYS & B-GIRLS {BREAKER DANCERS}.
Leo nabana sana kwa hii element ya 4 ambayo ni Breaker Dancer , kwa kifupi Historia ya Hip Hop Dancers ilianzia nchini Marekani miaka ya 70's ambapo vijana wengi walizoea ku-shake barabarani kwa kutumia midundo ya ngoma , na ilizidi kushika chat miaka ya 80's huku wakiimalisha uchezaji wao kwa kubuni style na mbinu mpya kila wakati.....

Kila kulipokucha ndio Dancing ikazidi kwenda next level kwa kubuni mitindo mipya na hasa kufanya mazoezi ya Breaking, Popping, Locking , Krumping na hata House dance, kitu kilichopelekea fani hii kushamili na kusambaa Dunia nzima ambapo kwa sasa ime - improve kwa kutumia vionjo vya JAZZ, ROCK, TAP na pia kwa kutumia hasa utamaduni wa kimarekani na kilatino katika kucheza.

Kwetu Tz na hata majirani zetu kanda za Afrika mashariki na kati bado utamaduni huu tunaubeza na kuuchukulia kawaida huku kukiwa na rundo la vijana wenye vipaji wakifa njaa na kupoteza mwelekeo wa maisha. Sanaa hii inapotea kwa kutopata kipaumbele ukilinganisha na michezo mingine ya kuburudisha . Na hata mashabiki wake ni wachache sana ukilinganisha na nchi nyingine zinazoendelea. TANZANIA HERE WE COME!!!!
By AGE'S Ent. stay tune......!!!!!

No comments:

Post a Comment