Friday, August 19, 2011

SKIN MPYA YA AZMA - BONGO FLEVA INAKUFA.

WAPENDWA!!! HUU NI WIMBO WANGU MPYA WA BONGO FLEVA INAKUFA,
NAOMBA SAPOTI YENU KATIKA BLOGS ZENU,REDIO ZENU NA KUWATUMIA MARAFIKI
NA WANAMUZIKI WOTE WA BONGO FLEVA WANAOPENDA KUSIKIA AU KUAMBIWA
UKWELI........MUNGU AWABARIKI KATIKA KAZI ZENU ZA KILA SIKU...

SONG: BONGO FLEVA INAKUFA
ARTIST: AZMA
EMAIL:azmamponda@gmail.com/umabe2010@yahoo.com
STUDIO: TATOO RECORDS.
PRODUCER: AK MUSIC/AK 47.
GENRE: HIP HOP
WEBSITE: www.umabearts.blogspot.com
COUNTRY: TANZANIA
LANGUAGE: KISWAHILI.
UMABE MEMBERS: AZMA MPONDA,VICTOR MRISHO,(KITA THE PRODUCER),GEORGE
OLOMI,FREDDIE NJEJE ETC..........

Intro:
Yah AK 47(ah ah), AZMA, (sure) I’.m not killing bongo flavor (yes
yes), bongo flavor wanajiua wenyewe.

Verse i
Ndugu zangu wapendwa,anzeni maandalizi ya msiba,
Bongo fleva imetendwa,sidhani kaa itapona kwa tiba,
Walio asi wanatengwa,mapengo yao yanazibwa,
Wengine wanachengwa,malengo yao,yanaibwa,

Wasanii hawana dira,wamepoteza mwelekeo,
Wanachezwa kama mpira,wakisubiri matokeo,
Mara hivi mara vile,hawaishi kwa upendo,
Mara hiki mara kile,kila siku ni skendo,

Wanauza sura za bandia,hawaishi maisha halisi,
Kila treni wana dandia,wanatamani kaa mafisi,
Kwa magari ya kuazima,wanang’oa mademu mtaani,
Wanauza sura kiulazima,wana mrehemu wasimlaani

Wamelala vitandani,mpaka inzi wame mkinai,
Wafungiwe vibandani,wana makosa ya jinai,
Wana mioyo iliyolaanika,hawaishi kwa divai,
Wengi wao wamelainika,ila mtaani wana jidai
Verse i
Hawana jipya,wakilala wakiamka ni mapenzi,
Hawana utu,ni mafala ni masnitch ni washenzi,
Wakiwa na shida wanakujali,wakipata tuu,wanajenga dharau,
Mtakutana ni kaa ajali, na ukiwafuata tuu,wameshakusahau,

Hawafai kabisa,nenda nao kwenu,,wakuharibie dada zako,
Wanachuki na visa,ukienda nao kwenu,watakuibia raba zako,
Wameshindwa kuuza mziki,na sasa wanauza sura,
Waliishi maisha ya dhiki, na sasa wamekuwa visura,

Wakiume wamejipodoa,wanongea kama mademu,na nywele wamesuka,
Wakike ni machangudoa, popote wanagawa gemu,na chati zina shuka,
Wakiimba wanalegeza macho na wanakata viuno,
Unaonyesha maungo yako,vipi upigwe mikuno?,

Ustaarabu hakuna,mtaani wanaranda randa kaa bidhaa za promotion,
Ukistaajabu nakuna,ushairi unawaganda ganda na kuwachana kislomotion,
Wakike wamekuwa vicheche,kawaulize ni mara ngapi wameshafanyiwa abortion,
Wakiume wanatema cheche,kila demu wanamtamani wanaendeshwa kwa emotion,

Verse iii
Naongea ili mjifunze,msiishie kunijadili,
Ni bora jamii ijitunze,isipoteze maadili,
Kila aliye na upeo, apewe kinachostahili,
Kwakuiga kwenye video hamtageuka mahili,

Ni kwa masela Fulani,mnao copy na kupaste,
It’s a tellor fun,mi ndio hopy mi ndio beste,

Nakuna,nawakomaza,waache uzembe kwenye gemu,
Hakuna ,wanachowaza,zaidi ya pombe na mademu,

Wanatia kinyaa,wanatisha kama mazimwi,
Wakikosa zinaa,hawatakosa kuwa naukimwi,
Daile wana sua sua,hawana kinga mwilini,
Hawawezi jina sua,wako empty akilini,

Wanapelekwa kwa maboya,hawanaga vision,
Wanamsifu tuu Latoya,hawanaga mission,
Kwa ajili yao,mziki wanaonekana kaa ni uhuni,
Hawana chao,wenye riziki tunawasweka kapuni,

Autro
yes yes AZMA ha ha AK 47,YES AH Thanx God, Mungu ibariki
TANZANIA,inusuru BONGO FLEVA,YES UMABE,I’m out nigaz.. THIS IS
HIPHOP.

SPECIAL THANX:
TO ALL THE FANZ OF AZMA & UMABE…..

IN GOD WE TRUST…
‘WE ARE THE BEST’

IN THIS PROFFESSION.


No comments:

Post a Comment