Friday, May 6, 2011

WEMA v/s BOB JOUNIR = MAHAKAMANI....... SO WHAT'S NEXT?????????

Bifu kati ya Miss TZ 2006 na Bob Jounir sasa lafika mbele ya Sheria, Wema Sepetu amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Mwanzo Kinondoni kwa kosa la kumtukana Raheem Rummy, Bob Jounir a.k.a Rais wa Masharobaro.

Wema (26) alikiri kutukana matusi hayo baada ya kuulizwa na hakimu kama mashitaka aliyosomewa ni kweli au si kweli. Kauli yake ilikuwa:- “Ni kweli nimemtukana lakini ilikuwa hasira tu,”.

Kesi itatajwa tena Mei 18 mwaka huu kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali na mshitakiwa yupo nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana.


Bifu kati ya Wema na Bob Jounir limetokana na chanzo cha Bifu ya Msanii Diamond ambaye ni mpenzi wake na Wema ambaye walikuwa na Bifu ya kisanii na Bob Jounir wiki chache zilizopita ambapo kwa mtazamo wangu niliona zinakuzwa na Media zetu.


Si mara ya kwanza kwa Wema kufikisha mbele ya Sheria kwani Miezi kadhaa iliyopita msichana huyo alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam kujibu mashitaka ya kuharibu gari la aliyekuwa mpenzi wake, Stephen Kanumba THE GREAT.

No comments:

Post a Comment