Monday, May 30, 2011

SEAN KINGSTON MAHUTUTI BAADA YA AJALI MBAYA!!!!!!!!


Hip-hop singer Sean Kingston kutoka MIAMI kahamishiwa ktk kitengo cha I.C.U (intensive care unit) Ktk Hospitali ya RYDER TRUMA CENTER baada ya kupata Ajali mbaya ya pikpiki ya maji (watercraft) kwenye daraja lililopo karibu na Miami Beach ... Msemaji wake kasema mapema leo asbh....

Kingston akiwa na demu mmoja wakiila bata za ufukweni kwa kudrive pikipik za majini walipata Ajali na kuumia vibaya baada ya pikipik ku-hit Daraja la Palm Island time za 12 jioni ya Jumapili ya trh 29 this May.............

Mamlaka husika zinaendelea kupeleleza kama Ajali hiyo imesababishwa na Bata wa kupitiliza "GAMBE" lakini mpk sasa hawajapata kielelezo chochote kuhusu hilo....


Jamaa tumwombee "Beautiful Gal Singer" Apone haraka haraka..... GET WELL SOON KINGSTON!!!!!!!!!

MISS UNIVERSE 2011 - NELLY KAMWELU.

Baada ya mchakato mzima wa kuwasaka mabinti kati yao apatikane wa kumrithi Hellen (Miss Universe 2010) Mwishowe Nelly Kamwelu kaibuka mshindi wa Miss Universe 2011......!!!


Kutoka Miss Tanzania mpaka Miss Universe.......................Daaaaaaaaaaaaaah!!!!! NEVER SAY NEVER... Hongera sana !!!
Hapa ni washindi watatu bora wa Miss Universe 2011.... Nakutakia mafanikio mema kwenye mashindano ya Miss Universe World ufanye poa zaidi ya Flav Matata.... God Bless Nelly, God Bless Tanzania!!!!!!!!!!!!

Thursday, May 26, 2011

HAPPY 1st B'DAY DEEN "THE NEXT BIG THING"


DEEN "The Next Big Thing" is the son of a Radio Host Ezden The Rocker. Today is a special day for friends and Family members, His first B'day since was Born!! Wish Him all the Best in His life..... And u really like to wish and know what's happening in Deen's world check him through Facebook...... ENJOY !!!!!!!!!!!!!!

Wednesday, May 25, 2011

C-SIR MADINI NEW ARTIST KUTOKA TETEMESHA.

Nachkua nafasi hii kukushkuru sana kwa support unayoendelea kutupatia kiukweli bila mchango wako hatuwezi fika popote.

Sisi kama TETEMESHA RECORDZ tumejiwekea malengo ya kuwa tunajaribu kutafuta wasanii wachanga kabisa lakini wenye vipaji na kuwapika kisha kuwatambulisha katika music industry hapa TZ.

Tulianza na HUSSEIN MACHOZI, akafuata SAJNA na sasa ni zamu ya msanii mwingine mpya C-SIR MADINI kutoka Mwanza

Huyu tunaemtambulisha sasa jina lake kamili ni PETER MPONEJA, na jina lake lingine la nyumbani ni MASISA, hilo MASISA lilikuwa jina la babu yake, na kutoka katika hilo ndio akaamua kulifupisha kuwa SISA na ndilo anatumia katika muziki lakini katika matumizi ya Muziki litakuwa likiandikwa C-SIR. ila kwa ukamilifu wake tunaomba mumpokee kwa majina mawili yaani C-SIR MADINI.Huu ndio wimbo wake wa kwanza kutoka, na utakuwa katika album yake ya kwanza ambayo bado tunaendelea kuirekodi. Video ya wimbo huu imekwishafanyika chini ya ADAM JUMA wa NEXT LEVEL na itatoka siku chache zijazo.


SONG'S DETAILS
Track Name: KIFUNGO HURU
Artist: C-SIR MADINI
lyrics composed by: C-SIR MADINI, KID BWOY & JOSEFLY
arranged by: C-SIR MADINI & KID BWOY
Produced by: KID BWOY
Mixed by: KID BWOY
Studio: TETEMESHA RECORDZ

Contacts: C-SIR MADINI: 0712-719004
KID BWOY: 0713-131073


Thanx for ur support.

Monday, May 23, 2011

R.I.P RAPPER WA CALI SWAG DISTRICT (M-BONE)


Mmoja wa member wa Cali Swag District ambao walivuma 2010 na Hit Song ya "Teach Me How To Dougie" aliyefamika kama Mante Talbert a.k.a M-Bone amefariki kwa kupigwa risasi alipokuwa ana-drive kwenye hometown yake Inglewood - California,(drive-by-shooting!)

M-Bone,alikua ni mmoja waliofanikisha hit song ya Cali Swag District,Teach Me How To Dougie Iliyotoka 2010, na inasemekana chanzo cha kifo chake ni ugomvi wa kugombea mwanamke na alipigwa risasi 2 kichwani na alipokimbizwa hospitali ,baadaye aliripotiwa amefariki dunia ......


Hapo kati ni member wanne wa Cali Swag District katika pozi ya pamoja. Mazishi ya M-Bone yatafanyika Ijumaa May 27,2011 pande za Faithful Central,Inglewood-California.


Mwenyezi Mungu ailaze Roho ya Marehemu M-Bone mahali pema peponi Amina!!!!!!!!!!!!!!!!

MISS UNIVERSE 2011 ON 27th MAY.

Compass Communications Co Ltd Tanzania Chini ya Director Maria Sarungi Tsehai Ndio waandaaji wa Miss Universe hapa Tanzania kila mwaka , na mwaka huu chini ya udhamini wa Vodacom Tanzania pale Golden Tulip Hotel ndio kitu kita-happen kutafuta mrithi wa Hellen..... who will be ????? Hutakiwi kumiss hapo kati tarehe 27 May this Furahi-Day.........
Hawa ni baadhi ya washiriki wa Miss Universe 2011 waliopatikana kutoka mikoa tofauti tofauti ya Tanzania, na mmoja kati yao ndio atakuwa mshindi na kumrithi wa Hellen.....
Hapa washiriki wakipata maelezo ya mfanayakazi/mwakilishi wa Vodacom Tanzania walipotembelea Vodashop pale Mlimani City


Wanafamilia ya Compass Communications Co Ltd Tanzania, Mario (Mr Tanzania 2010/2011), Hellen (Miss Universe 2010/2011) huyo bro sijamsoma vizuri na Maria Sarungi Tsehai (Director).........


Hii sio ya kukosa pale Golden Tulip Hotel siku ya Friday ya Tarehe ya 27 May...... !!!

Monday, May 16, 2011

PROF JAY NA UJIO MPYA... "KAMA IPO"

Baada ya kuwa kimya kwa miaka kadhaa mtu mzima kwenye game la bongo fleva Joseph Haule aka Prof Jay aka Dad aka amerudi tena na wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la KAMA IPO.

Wimbo huu mpya umetengenezwa katika studio ya FishCrub pale kati k/koo chini ya Producer Lamar.


Sikiliza wimbo huu mpya wa Prof Jay then tupia hapo kati ujio wake umeuonaje?.

NIKKI MBISHI ONCE AGAIN WITH NEW HIT GOES BY "SAUTI YA JOGOO"

If you carefully analyze his released songs, you will realize that NIKKI MBISHI always come with a surprise gem which later become a star. He started with his debut song “PUNCHLINES” where surprise package was GRACE MATATA (first song her voice to be heard on the radio), then his second release “KILA SIKU” which also featured by Belle 9 and Godzilla was an opportunity for the introduction of ONE THE INCREDIBLE. The third radio release material for the self proclaimed king of freestyle “PLAYABOY” was the platform for BEN POL to introduce his voice on the media. Now he is coming with the new gem “bella”.

The talented singer, one of the THT rpoduct, was one of the previous BSS finalists; she is now a member of machozi band and also working on her solo album. This song was recorded early last year, by that time Bella was not on the map, Nikki is still proving that not only he is one of the best hip-hop stars of his generation but also he has a good ear. Music lab is glad to introduce his new joint “Sauti Jogoo” featuring Bella & Maulo, below are the details:
Song title: Sauti ya jogoo

Artist: Nikki mbishi

Written by: Nikki mbishi, Maulo & bella kombo

Produced & mixed By: Duketachez for Music lab

SIKILIZA HILO GOMA HAPO THEN TUPIA CHOCHOTE....

Thursday, May 12, 2011

LIBENEKE JIPYA KONA YA MATUKIO..

Tunapenda kulitambulisha wadau wote libeneke jipya la KONA YA MATUKIO ambapo nia na lengo kubwa ni kuleta matukio yanayotokea kila siku katika Jamii yetu na Duniani kwa Ujumla..pia kutakuwa na Matukio ya papo kwa hapo yani Breaking News Endelea kuwepo kila muda kujua nini kitatokea

Kama unatukio la aina yoyote tutumie kupitia tonemultimediacoltd@yahoo.com karibuni nyote na asanteni kwa kututembelea.

Pamoja Tunaweza


LINK: www.konayamatukio.blogspot.com

Wednesday, May 11, 2011

THE ROCKING WEDDING on 6May 2011...

Kama ndio mara ya kwanza kutupia sura hii kwa macho yako !! Okey Goes by the name of Ezden Jumanne Presenter wa Kiss Fm kutoka Rock City....... Funz wake knows him kama The Rocker kupitia Show ya Kiss Collabo MixX ya Kiss Fm For Today's Best Music.... Na pia kwenye Supa TraxX ya Star Tv.......

So jamaa katoa kipigo na kuacha Pengo kwenye Kambi ya makapera baada ya juzi kati ku-tie knot na mwandani wake wa siku kibao MAMA DEEN.........Mr. & Mrs. Ezdan the Rocker wakiingia ukumbini ..... ready to .....

Orginal Jumanne akiwa na Mrs wake na mjukuu wao Deen wakitoa wasaha kwa wana.

NIPE...............

NIKUPE...........


DANCING........


SHOW LOVE NA WANA...........

ALL THE BEST BRO......... UMEFUNGUA NJIA SISI PIA TWAKUFATA NYUMA YAKO.

BOB MARLEY'S DAY... R.I.P


Alijulika kama Nesta Robert "Bob" Marley, OM (6 February 1945 – 11 May 1981) akiwa mwimbaji, mwandishi na mwanamuziki toka Jamaica. Pia Bob alikuwa rhythm guitarist na aliongoza kuimba kwenye ska, rocksteady & reggae band Bob Marley & The Wailers (1963–1981). Marley anabakia kuwa the most widely known & revered performer wa muziki wa reggae, pia anasifika kwa kusaidia Ku-spread Movement za Jamaican music & Rastafari worldwide.Muziki wa Bob ulikuwa unatoka na mambo ya kijamii yanayotokea Jamaica, na inafahamika kuwa alilenga sana kutoa sauti has kwa mambo ya Siasa na Tamaduni za Jamaica.

Na kati ya ngoma kali ambazo azitasahaulika za Bob ni "I Shot the Sheriff", "No Woman, No Cry", "Could You Be Loved", "Stir It Up", "Jamming", "Redemption Song", "One Love" and, together with The Wailers, "Three Little Birds", "Buffalo Soldier" & "Iron Lion Zion". The compilation album Legend (1984), ambayo iliachiwa miaka mitatu baada ya kifo chake, kuwa Albamu ya reggae's best-selling , ikifika mara kumi kwa mauzo ya Platinum (Diamond) huko U.S., na kuuza copy 25 million worldwide.

TUTAKUKUMBUKA SANA BOB MARLEY KWA MCHANGO WAKO !!! R.I.P

Friday, May 6, 2011

BATA KILA SEHEMU.... WELCUM 2 MY HOODWEMA v/s BOB JOUNIR = MAHAKAMANI....... SO WHAT'S NEXT?????????

Bifu kati ya Miss TZ 2006 na Bob Jounir sasa lafika mbele ya Sheria, Wema Sepetu amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Mwanzo Kinondoni kwa kosa la kumtukana Raheem Rummy, Bob Jounir a.k.a Rais wa Masharobaro.

Wema (26) alikiri kutukana matusi hayo baada ya kuulizwa na hakimu kama mashitaka aliyosomewa ni kweli au si kweli. Kauli yake ilikuwa:- “Ni kweli nimemtukana lakini ilikuwa hasira tu,”.

Kesi itatajwa tena Mei 18 mwaka huu kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali na mshitakiwa yupo nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana.


Bifu kati ya Wema na Bob Jounir limetokana na chanzo cha Bifu ya Msanii Diamond ambaye ni mpenzi wake na Wema ambaye walikuwa na Bifu ya kisanii na Bob Jounir wiki chache zilizopita ambapo kwa mtazamo wangu niliona zinakuzwa na Media zetu.


Si mara ya kwanza kwa Wema kufikisha mbele ya Sheria kwani Miezi kadhaa iliyopita msichana huyo alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam kujibu mashitaka ya kuharibu gari la aliyekuwa mpenzi wake, Stephen Kanumba THE GREAT.

Tuesday, May 3, 2011

MSHINDI WA TUNZO YA TEENIES CHOICE AKUMBWA NA SKENDO YA USAGAJI


Anafamika kama Judith Nyambura Mwangi, 23 yrs Old Singer, Poet, Designer, Painter Kutoka katika industry ya Music Kenya anafahamika zaidi kama Avril ambaye hivi karibuni ka-sign na Ogopa deejays production House. Kwa kifupi Avril kwa sasa anapiga Degree ya design pale kati University of Nairobi.

Kama unamkumbuka Avril Amewahi kushikisha na A.Y kwenye RMX ya ngoma "LEO" na pia ana Single yake inaitwa "MAMA" huku pia akiwa amepewa shavu kwenye ngoma ya Jaguar kwenye Track inayokwenda kwa jina la Tayari .Daaaah umemsoma Avril, LETS BACK TO THE TOPIC..........................................Kuna pix kibao kwenye mitandao kibao kuhusu huyu binti Mrembo ambaye zinamwonyesha akifanya mambo za kisagaji. moja wapo ni hii hapa chini..


..............Kuna baadhi ya picha siwezi kuzi-post kutokana na suala la Maadili yetu, Pia juzi juzi tu alishinda tunzo ya Teenies Choice huko kenya........ Je hii hali pia Bongo inashika kasi kwa wasanii wetu wa kike?