Wednesday, April 6, 2011

PIPI KUPEPERUSHA FLAG YA TZ WORLD WIDE.

Ni moja kati ya Underground ninayemkubali toka mara kwanza kumsikia kupitia ngoma ya Njia panda ya Barnaba. Kutoka THT ilifahamika kama PIPI lakini mie namtambua kama Doreen binti mwenye Hustlement za uhakika na hasie kata Tamaa.

Leo asbh nilipokea msg kutoka kwa Pipi akinitaka Raia na Fans wake kujua nini kinaendelea kuhusu yeye ambapo alifunguka kama ifuatanvyo:-


"MAMBO? MWEZI WA PILI TAREHE 29 NILISHIRIKI KATIKA AUDITION YA ORGANISATION MOJA YA KIMATAIFA INAITWA UMOJA FLYING CARPET AMBAYO ILIKUWA INATAFUTA VOCALISTS, DANCERS AND MUSICIANS.....WATU 15 NDO WALIOHITAJIKA NA NILIBAHATIKA KUWA KATI YA WAIMBAJI WANNE TULIOCHAGULIWA.... BINAFSI NAONA KAMA MIUJIZA KWANI SIKUTARAJIA KWAMBA NITAANZA KUONEKANA KIMATAIFA MAPEMA HIVI KWANI TOUR HII ITANIWEZESHA KUKITANGAZA KIPAJI CHANGU NCHI MBALIMBALI KAMA UGANDA, ETHIOPIA, MOZAMBIQUE,NORWAY, NETHERLANDS NA SOUTH AFRICA..... NA PIA NAAMINI HUU NI MWANZO MZURI KATIKA JITIHADA ZA KUITANGAZA BENDERA YA NCHI YANGU KUPITIA KIPAJI CHANGU..." alimalizia Pipi.


Huu ni mwanzo mzuri kwake na kwa Watanzania wote . So Pipi mimi nakutakia Mafanikio Mema fanya tu kuiwakilisha Bongo for real. ALL THE BEST PIPI.

No comments:

Post a Comment