Wednesday, March 23, 2011

NI TANZANIA URBAN MUSIC OR TANZANIA FLEVA UNIT???

MR. II a.k.a Sugu mwakilishi wa Tanzania Urban Music (TUMA), ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya mjini. Tuma ni chama cha wasanii wa Muziki wa kizazi kilichosajiliwa kisheria na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA).

Mkubwa Said Fella Mwakilishi wa FLEVA UNIT, ambaye pia ni kiongozi wa kundi la TMK WANAUME lenye makazi yake Temeke jijini Dsm. FLEVA UNIT ni kampuni ambayo imesajiliwa na msajili wa makampuni Nchini (BRELA).
Mpaka hapa me bado najiuliza mwisho wa hili ni nini???? Hii ni baada ya mchakato na malumbano ya muda Mrefu kuhusu Mastering Studio aliotoa Mh. JK kwa wasanii miaka mitatu iliyopita.
Kwa mujibu wa Vyanzo vya Habari ni kuwa Fleva Unit ilipewa Usajili wiki moja iliyopita, Je swali ni kuwa muda wote huo nini kilikuwa kinaendelea? na hivyo vifaa vilikuwa wapi? Kwa mujibu wa Katibu Mtendaji wa BASATA Bw. Materego anasema TUMA ndio chama pekee kinachotambulika na BASATA.
JK katoa msimamo wake kuhusu Studio hiyo kuwa aliitoa kwa watu waliomuomba . Je huu msimamo na Kauli ya Mh. JK iliyowakilishwa na Mkurugenzi Msaidizi Sanaa Bi. Ngowi inalenga nini ? Tulitumaini kupata Umoja wa wasanii Tz kwa maendeleo ya Muziki wa Kikazi Kipya kwani Rais ni wa Watanzania Wote!!! Nilitegemea hiyo Studio ingewekewa utaratibu ili iwasaidie Wasanii wote na sio waliomba tu kwani wote wanaihitaji huo msaada.
Kwa mtazamo wangu mpaka hapo Tumeshajenga makundi katikati ya INDUSTRY na hata inaweza kuleta uhasama kati yetu. Muziki huu bado una matatizo mengi sana so kama tumeanza hapa kwa hivi tutayamaliza?????????????
Ni jukumu la WIZARA husika na BASATA kuokoa hili JAHAZI na si vinginevyo!!!!!!!!!!!!!!

No comments:

Post a Comment