Monday, March 28, 2011

JAY DEE AFUNGUKA NA TUNZO ZA KTMA 2011

Sikuweza kufika kwenye tuzo za Kili kwakuwa sikupatiwa mwaliko, niliogopa kuzamia. Nadhani walinisahau.........Tehe tehe tehe Hata mwakilishi wangu yoyote pia hakuwepo ila Shabiki mmoja wapo alinipokelea na kuniletea Nyumbani Lounge. La muhimu zaidi nashukuru sana Watanzania wote mlionipigia kura, sina cha kuwalipa zaidi ya Asante. Nashukuru wote mnaoendelea kuamini kuhusu JayDee Tuko pamoja siku zote.
Bahasha imeandikwa Mwimbaji Bora wa Kike, ambayo kwa kidhungu nadhani ni Best Female Vocalist. Tuzo hiyo alipewa mtu mwingine Linah wa THT.


Tuzo niliopewa mimi iliandikwa Female Artist of the Year ambayo ni Msanii Bora wa Kike wa Mwaka. Nadhani ubinaadam tu hapo umepita kama kuna fotauti na imani zitarekebishwa, kama yangu ina mpunga zaidi basi wataniongezea tu! Wink!!


Bahasha ya kwanza inanihusu nahakika ila ya pili ilioandikwa Best East African song sina hakika sana kama tunagawana na Kidum au kila mtu kapewa ya kwake??? Sina taarifa za undani, itabidi mzigo niuhifadhi nisijeanza kuutumbua mara naambiwa si zangu Mwaka Flani hivi nakumbuka wimbo wa Anita niliofanya na Matonya ulipata kuwa Wimbo bora wa Mwaka zikatoka Trophies 2 na kila mtu akapata fungu la pesa kiasi.


Sijajua kama na kwa wimbo huu niliofanya na Kidum itakuwa hivyo au mwaka huu ni tofauti manake kila mwaka mambo huwa yanabadilika kwenye Tuzo hizi

Huyu ni shabiki wa Machozi Band na Jay Dee aliyejitoa muhanga kwenda kupokea Tunzo za Jay Dee......... Info zaidi tembelea www.ladyjaydee.blogspot.com

No comments:

Post a Comment