Tuesday, January 4, 2011

THIS IS FOR MY PEOPLE ALL OVER DA WORLD. 2011

Kwa mara ya kwanza 2011 najitokeza na kutoa Shukrani zangu Kwa Yule aliye Juu (Mungu Baba) kwa kunifikisha kuuona mwaka huu wa neema 2011 kama wengi wanavyoutabiria. Asante Eeeeeh Mungu uliye juu...

Pili Shukrani zangu nazidondosha kwako wewe mdau wa tasnia ya Burudani hasa Muziki wetu wa kizazi kipya kwa kunipatia Support ya namna moja au nyingine kwa kipindi chote cha 2010
hasa kwa kutembelea Blog hii, kutazama kipindi changu (Kwa wale mnaoshika Tumaini Tv) cha Tupo Pamoja na hasa wale wadau mliokua mnanipatia maoni na ushauri mbalimbali ktk mchakato mzima wa kuendeleza Bongo Music Industry 2 next Level..... Ni ngumu sana kuwataja kwa majina wote lakini popote ulipo Asante saaaaaaana.....
Tatu ni kwa Wazazi wangu wapendwa kwa support ya kunitia moyo kuwa naweza na kuwa proud of Me kwa kila nachofanya kwa mwaka wote, Ndg, Jamaa na Marafiki zangu wa karibu. Hasa kwa Wafanyakazi Wenzangu Hapa Ebony Fm (Dar & Iringa) na pia wale wa Tumaini Tv kwa support toka nimeanza mzigo kwa mwaka wa 2009/2010. Mungu Awabariki saaaana.
Mwaka mpya huu wa 2011 ni mwaka wa MAPINDUZI kwangu na hata kwa jamii nzima ya kitanzania (Namanisha Mwaka wa Kihistoria ). Kwanza ni mwaka ambao tutaazimisha miaka 50 ya Uhuru hapo Dec 09, Pia ni mwaka ambao Watanzania wengi tunategema kupata Katiba mpya (Kama azimio litafanyiwa kazi) na Upande wa Bongo Music Industry ni mwaka wa kucheka kwani tumempata Mwakilishi atakae peleka kilio chetu cha Mda Mrefu Bungeni (Mh. Sugu) kwa kuamini mambo yatakaa sawa. Na mwisho naamini mafanikio yaliojitokeza 2010 ktk Muziki hayataishia hapo.... So Vijana wenzangu itz our Time embuuu tupigeni kazi kwa Bidii kulijenga Taifa Letu kwa Historia ya wajukuu zetu...
Nawatakia Baraka Tele na Mafanikio zaidi kwa mwaka 2011, Bila Kumsahau mmiliki wa pumzi yako kwa kila Jambo Unalotenda (Mwenyezi Mungu).. Mungu mbariki Arnie Gizzle, Mungu bariki Muziki kizazi kipya, Mungu Ibariki Tanzania, AMINA!!!!!!!!!!!!!

No comments:

Post a Comment