Wednesday, January 5, 2011

NAFUNGUKA NA DOGO JANJA KWA KUANZA MWAKA 2011..

Sema Ngare Narooooooooooooooooh, Nikisema Dogo wewe Sema Janja... Haya Dogo............., Dogo.........., Dogo........., Dogo......., Haaa hah aha hah hah aha hah aha!!!!!!!!!!!!!!!!! Anajua ndio maana wamemchukua ...... Ni mjanja zaidi ya Janja Alais Abudalazizi Chende ambaye ni msanii mdogo sana mwenye kipaji kikubwa cha kuimba, anayekuja kwa kasi ya ajabu katika fani ya muziki kwa mwaka 2011 ambapo kwa sasa yupo chini ya wakali wa Tip Top connection.

Kwa mwaka huu me naanza kwa kufunguka na Dogo huyu mwenye Under 15 yrz old. Kama kuna vitu ambavyo vimenifanya nione Feeling zangu na love yangu kwenye muziki imetendewa Haki ni pale Nilipomwona Dogo anatupia free style ktk Tamasha moja lilofanyika mwishoni mwa mwaka jana (2o1o)... Kwa tadhimini ya haraka nikajua mmmmh!! 2011 wakongwe watasoma namba..... Kinachoniua ni utamshi wake wa maneno (Daa swagga za A-tOWn)........

Kwa sasa Dogo kadondosha ngoma mpya akiwa na King wa Salasala GodZilla Inayokwenda kwa jina la "IF I GET MONEY" embuuuuu tupia sikio hapo pembeni kwenye Blog.......

Kwa ngoma ambayo imemaliza mwaka 2010 poa na inazidi fanya poa kila siku ya 2011 ANAJUA.... kUNA VERSE moja Dogo Katupia kila nikiisikia nashindwa msoma... Labda wewe utaweza embuuuuuu tupia Jicho lako ....."Kibaka kakaba kahaba kaiba mkoba katika mkoba kakuta kiroba kakuta kizoba kakuta ratiba msiba hehehe uyoo kakuta ratiba msiba"..........


Dogo Mwaka umeunza poa kwako na nina matumaini utaumaliza poa sana.. So nakutakia Mafanikio Mema bila kusahau Skonga,, si unajua Elimu na Muziki inakuwa poang'a sana kama Nikki wa Pili n.k

No comments:

Post a Comment