Friday, January 28, 2011

HAPPY BIRTHDAY EDDO THE AMBASSADOR..


Kutoka Nyanda za juu Kusini ni Balozi Eddo Bashir , Mtoto aliyezaliwa siku kama ya Leo, So point ya msingi hapa ni Pamoja Tumtakie Maisha Marefu huyu King of The Southern Highland kupitia Bonge bonge moja la Afternoon Show Goes by the Name of THE SPLASH... Hayaaaaaaaaaa kupitia Radio ya Ukweli EBONY FM. Ni Presenter shupavu ambaye ukijaribu kusikiliza Show yake hutajaribu kui-miss Kamwe!!!!!!... Watu wangu wa Mbeya, Iringa na kote huko Nyanda za Juu Kusini Mnaisoma Hii Namba So wote tufanye hiviiiiiiiiii HAPPY B'DAY OUR AMBASSADOR!!!!!!

Friday, January 21, 2011

NYANDA ZA JUU KUSINI GET READY ,,,,!!! KEY TO THE WEEK END.Peopleeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee this is Kija's 15,, So soon kupitia Ebony Fm.. daah kama kaa mkao wa kula hizi bata pande hizo straight from Dar es Salaam...................

Ntakujuza zaidi itakuwaje hapo kati, Nice Week End wadau kabla Umeme hujakatika!!!!!!!!!!!

Tuesday, January 18, 2011

"AM THE BEST 2010".. COMEDIAN MWALUBADU.

From Iringa Town Tanzania, goes by the name of Athman Mussa Mwalubadu ambaye anamake-headline kwenye Best Leading Radio Station in Southern Highland (u know what i mean?) Ebony Fm, Amenyakua Tunzo ya kuwa Mchekeshaji Bora wa mwaka 2010 kutoka Film Central Awards..... Ambao ni mtandao bora wa kutangaza kazi za filamu hapa Bongo........ HONGERA SANA KAKA.

Si tuuu ni mfanyakazi mwenzangu but all da time nikimwona huyu jamaa najisikia Kupasuka mbavu aisee....... Kwa wale mnaomfahamu hope u knw what i mean? Embuu tafuta comedy Movie inaitwa INYE NDEMB'WENDEMB'WE Utaniambia kama kweli anafaa kutwaa hiyo Tunzo au vipi?

Monday, January 17, 2011

FROM THE HOOD.....HAPPY BIRTHDAY BRO KIJA 15.

Hakuna siku tamuuuu kama siku ya kuzaliwa kwako hasa pale unapoitambua umuhimu wake kama ambavyo Renatus Kiluvia A.k.a Bizzo au Kija 15 alivyoitambua siku yake LeO...... Daaaaaaaaaah many wishes to my Bro frm the Hood na Mfanyakazi mwenzangu pale kati Ebony Fm Branch ya Dsm .. Jamaa all the Best Mwana PAMOJA DAIMA KAMA www.muzikinamaisha.blogspot.com humo ndimo anamokaa fanya kumchungulia hapo katikati...

Saturday, January 15, 2011

TEDDY KALONGA "TK" KAINGIZA MZIGO WAKE MWENYEWE SOKONI.

Hii kwangu na mtu yoyote mpenda maendeleo ni hatua kubwa kwa Mtanzania mwenzetu na ni mfano wa kuigwa.... So sina budi kumwambia TK Hongera sana kwa kuingiza mzigo kama huu sokoni... MY LOTION ndio jina na hapo juu ni baadhi ya vitu vinavyotumika kuitengeneza .
Hapa ni TK na Huby wake wakila good time. NAMNUKUU MANENO YAKE.... "Biblia inasema, wote wamtiiyo bwana atawabariki mjini, mashambani, kazi za mikono yao, na hata kizazi chao chote! Mungu ameibariki ndoa yangu, biashara yangu, na mikono yangu. Nina good news kutoka kwa rafiki na mteja wa MyLotion. Wateja wengi hupenda MyLotion yenye Lemon scent, wanasema wakijipaka hawahitaji perfume. Pia kuna wanaopenda MyLotion yenye Vanilla scent."TK" ..." Mwisho wa kunukuu.

Mzigo ndio kama huu unavyoonekana So wadada kama unautaka very Simple sana fanya tuu kubofya hapa Chini....
Ukitaka kununu lotion hiyo tembelea
www.mylotionbytk.blogspot.com

Tuesday, January 11, 2011

KUTOKA THT MPK MLIMANI CITY,, ALBAMU KALI KUZINDULIWA LEO.

Hii ni ya Amininayokwenda kwa jina YAMETEKA DUNIA.
Hapa ni mzigo ATATAMANI ya mwanadada Linah...
Mzee wa viduku style Mataluma na mzigo mkali wa MAMA MUBAYA ..
Design kama jina la Albamu linaendana na mzigo mkali kutoka kwa huyu jamaa mwenye Vipaji lukuki Barnaba ... Nani hasiyekubali kuwa KICHWA CHAKE kikali?
Zamani ka dogo Ditto hila kwa sasa ni Ditto anafunguka na mzigo wake wa WAPO.......
Kama si ya kukosa hivi leo pale kati Mlimani City huku wakisindikizwa na wana kibao.
Tukutane pale wadau!!!!!!!!!!!!!

BLUE UMECHEMKA MBAYA VIDEO YA TUKO PAMOJA.

kati ya vitu napenda ni kuwa mkweli linapokuja suala la maendeleo ya muziki wetu wa kizazi kipya. Kwa mwaka huu 2011 msanii wa kwanza kufanya video mbaya ni Mr.Blue a.k.a Kabyser aliyoifanyia production moja ya (uchochoro) South Africa.

Jamaa ka Blue sikutegemea kama anaweza shusha P yake kwa kusambaza home use Video kwenye Media kwa ajili ya Air Time.... Daaaah Embu angalia Video yake ya mwisho ya Tabasamu iliyofanywa na Kallaghe then angalia hiyo mpya ya Tuko Pamoja utanipa jibu lako hapa...

Sijui kanzenguka na S.Africa nini? kwani hana washauri jamaaa.. Qulity mbovuuuuuuuuuuuu!!! ni mtazamo ka ujaiona fanya kuitafuta kwa yotube au www.bongostarlink.com

Wednesday, January 5, 2011

BONGO HIP HOP ICON OF ALL TIME NDANI YA BILLZ THIS SUNDAY.

Hii si ya kukosa ,, Ni mkali wa free style, lyrics zenye Ujazo, stage Perfomance ya hali ya juu na swaga za kutosha namwiita Bongo Hip Hop Icon of All Time ... Fid Q.. So usikose this Sunday pale Club Billz akitupia Bonge moja la Albamu bum bum of the century goes by the name Propaganda...

NAFUNGUKA NA DOGO JANJA KWA KUANZA MWAKA 2011..

Sema Ngare Narooooooooooooooooh, Nikisema Dogo wewe Sema Janja... Haya Dogo............., Dogo.........., Dogo........., Dogo......., Haaa hah aha hah hah aha hah aha!!!!!!!!!!!!!!!!! Anajua ndio maana wamemchukua ...... Ni mjanja zaidi ya Janja Alais Abudalazizi Chende ambaye ni msanii mdogo sana mwenye kipaji kikubwa cha kuimba, anayekuja kwa kasi ya ajabu katika fani ya muziki kwa mwaka 2011 ambapo kwa sasa yupo chini ya wakali wa Tip Top connection.

Kwa mwaka huu me naanza kwa kufunguka na Dogo huyu mwenye Under 15 yrz old. Kama kuna vitu ambavyo vimenifanya nione Feeling zangu na love yangu kwenye muziki imetendewa Haki ni pale Nilipomwona Dogo anatupia free style ktk Tamasha moja lilofanyika mwishoni mwa mwaka jana (2o1o)... Kwa tadhimini ya haraka nikajua mmmmh!! 2011 wakongwe watasoma namba..... Kinachoniua ni utamshi wake wa maneno (Daa swagga za A-tOWn)........

Kwa sasa Dogo kadondosha ngoma mpya akiwa na King wa Salasala GodZilla Inayokwenda kwa jina la "IF I GET MONEY" embuuuuu tupia sikio hapo pembeni kwenye Blog.......

Kwa ngoma ambayo imemaliza mwaka 2010 poa na inazidi fanya poa kila siku ya 2011 ANAJUA.... kUNA VERSE moja Dogo Katupia kila nikiisikia nashindwa msoma... Labda wewe utaweza embuuuuuu tupia Jicho lako ....."Kibaka kakaba kahaba kaiba mkoba katika mkoba kakuta kiroba kakuta kizoba kakuta ratiba msiba hehehe uyoo kakuta ratiba msiba"..........


Dogo Mwaka umeunza poa kwako na nina matumaini utaumaliza poa sana.. So nakutakia Mafanikio Mema bila kusahau Skonga,, si unajua Elimu na Muziki inakuwa poang'a sana kama Nikki wa Pili n.k

Tuesday, January 4, 2011

THIS IS FOR MY PEOPLE ALL OVER DA WORLD. 2011

Kwa mara ya kwanza 2011 najitokeza na kutoa Shukrani zangu Kwa Yule aliye Juu (Mungu Baba) kwa kunifikisha kuuona mwaka huu wa neema 2011 kama wengi wanavyoutabiria. Asante Eeeeeh Mungu uliye juu...

Pili Shukrani zangu nazidondosha kwako wewe mdau wa tasnia ya Burudani hasa Muziki wetu wa kizazi kipya kwa kunipatia Support ya namna moja au nyingine kwa kipindi chote cha 2010
hasa kwa kutembelea Blog hii, kutazama kipindi changu (Kwa wale mnaoshika Tumaini Tv) cha Tupo Pamoja na hasa wale wadau mliokua mnanipatia maoni na ushauri mbalimbali ktk mchakato mzima wa kuendeleza Bongo Music Industry 2 next Level..... Ni ngumu sana kuwataja kwa majina wote lakini popote ulipo Asante saaaaaaana.....
Tatu ni kwa Wazazi wangu wapendwa kwa support ya kunitia moyo kuwa naweza na kuwa proud of Me kwa kila nachofanya kwa mwaka wote, Ndg, Jamaa na Marafiki zangu wa karibu. Hasa kwa Wafanyakazi Wenzangu Hapa Ebony Fm (Dar & Iringa) na pia wale wa Tumaini Tv kwa support toka nimeanza mzigo kwa mwaka wa 2009/2010. Mungu Awabariki saaaana.
Mwaka mpya huu wa 2011 ni mwaka wa MAPINDUZI kwangu na hata kwa jamii nzima ya kitanzania (Namanisha Mwaka wa Kihistoria ). Kwanza ni mwaka ambao tutaazimisha miaka 50 ya Uhuru hapo Dec 09, Pia ni mwaka ambao Watanzania wengi tunategema kupata Katiba mpya (Kama azimio litafanyiwa kazi) na Upande wa Bongo Music Industry ni mwaka wa kucheka kwani tumempata Mwakilishi atakae peleka kilio chetu cha Mda Mrefu Bungeni (Mh. Sugu) kwa kuamini mambo yatakaa sawa. Na mwisho naamini mafanikio yaliojitokeza 2010 ktk Muziki hayataishia hapo.... So Vijana wenzangu itz our Time embuuu tupigeni kazi kwa Bidii kulijenga Taifa Letu kwa Historia ya wajukuu zetu...
Nawatakia Baraka Tele na Mafanikio zaidi kwa mwaka 2011, Bila Kumsahau mmiliki wa pumzi yako kwa kila Jambo Unalotenda (Mwenyezi Mungu).. Mungu mbariki Arnie Gizzle, Mungu bariki Muziki kizazi kipya, Mungu Ibariki Tanzania, AMINA!!!!!!!!!!!!!