Friday, December 10, 2010

TANZANIA VOTE FOR DIAMOND MTV MAMA AFRICA AWARDS.URBAN PULSE CREATIVE Inawaomba na kuwasihi watanzania wote pale walipo kuwa wazalendo na kumpigia kura Mtanzania mwenzetu, Ndugu Yetu, rafiki Yetu, Msanii wetu mpendwa Diamond ambaye amebahatika kuwa miongoni mwa wasanii wachache waliochaguliwa kuwania Tuzo za MTV MAMA AFRICA Awards Zitakazo fanyika Nigeria Jijini Lagos Jumamosi hii 11.12.10

Hivyo Basi watanzania na wadau wote wa muziki mnaombwa sana kupiga kura ili Kumwenzesha Diamond ashinde tuzo hii muhimu iweze kuja Tanzania ili kuiwezesha Nchi yetu kujulikana zaidi ulimwenguni na pia kuleta HESHIMA kubwa kwa kila MTANZANIA.

Namna ya kupiga Kura ni kama ifuatavyo:
1. Kwa njia ya simu unaweza kupiga kura yako kwa kuandika neno BNA DIAMOND kisha tuma text kwenda namba 6262, kwa walio nje yaTanzani tuma text 15726.

2. Kutumia Mtandao tembelea tovuti hii http://www.mtvbase.com/splash/mama/ bonyeza mtv mama halafu ingia ndani ya nominees tunaomba umpigie kura as the best New Act.

Tafadhari fanya sehemu yako pia mwambie na mwenzako.
Asanteni sana Mungu awabariki.

Diamond Platinumz
akishirikiana na
URBAN PULSE CREATIVE

No comments:

Post a Comment