Monday, November 8, 2010

MTIKISIKO 2010 ULIVYOTIKISA JIJI LA MBEYA.


Hapa ni uwanja wa sokoine pale kati Mbeya city a.k.a The Green City ikiwa ni maandalizi ya mwisho ya Stage ya Ebony Fm the # 1 Radio in Southern Highland . Bonge moja la tamasha kwa Udhamini mkubwa wa kampuni ya simu za mkononi Vodacom na kampuni ya bia TBL kupitia Brand ya Kilimanjaro premium Lager.

Daah wana Mbeya City walijitokeza kwa wingi sana kumla Bata mrefuuuuuuuuuu pande hizo kama wanavyoonekana hapo kati.
Kati ni wana Twanga pepeta kisima cha Burudani wakisugua kisigino kwa wana Mbeya waliojitokeza kwa wingi kumla Bata Mrefuuuu........... daaaaaah palikuwa hapatoshi bana. Never happen in the History of Mbeya!!!!!!!!!!!!!

Anaitwa Dj Muba all the way from Iringa Town (Ebony Fm) to Mbeya City kwa ajili ya kitu kimoja tuuuu.... kusugua lp ili kufanikisha na kuhakikisha Bata wa Mtikisiko 2010 anakuwa Mrefuu na analiwa Vizuri saaana bana na people wa Mbeya.


Kutoka Jumba la Vipaji Tanzania (THT) Hapo kati Linnah akiwa anamwimbia Dude wa Mbeya kuwa akimwona amponde mawe ...ullishaisoma eeeeeeeeeeeeeeh!!Palikuwa hapatoshi kipindi stage ilipovamiwa na mtu mzima wa hii ni Tanzania , Namzungumzia Roma ambaye alionekana kuwapagawisha watu wa mbeya ile mbaya.... walipata wazimu wa muda mpk basi hasa pale alipoimba ngoma yake ya Tanzania.
Hawa jamaa walitisha mbaya sana kwani waliingia na support ya kutaja sana jina la Sugu Mp mteuliwa wa Mbeya na kufanya Uwanja mzima kupiga kelele mbayaaa... Nawazungumzia TMK wanaume Halisi wakiongozwa na Sir Nature.
Hapa kati ni mtu mzima Sir Nature akishow love stajini kwa wana wa Mbeya waliofika kula Bata mrefuu pale kati uwanja wa Sokoine..... Jamaa walipiga kelele mwanzo mwisho mpk jamaa anashuka stejini walikuwa wanataka aendelee kuwapa bata .
Baadae wakapanda Chegge na Mh. Temba wakiweka mkono mmoja juu na wana Mbeya wakaweka mkono juu huku wakila bata mrefuu, Wasanii kibao walikuwepo pande hizo kukamilisha Tamasha la Mtikisiko 2010 pande za Mbeya City, Ambao ni BARNABA, IZZO B, LINEX, MIKE TEE N.K huku wakisindikizwa na wasanii wa Mbeya......................................

Sasa bata Mrefuu anahamia Iringa Jumamosi hii trh 13/11/2010 pale uwanja wa Samora huku wakiwepo weasal n' Radio frm Uganda,. Ebony Fm FEEL THE DIFFERENCE !!!!!!!!!!!!!!!!!

No comments:

Post a Comment