Thursday, September 30, 2010

TUPO PAMOJA SEASON II, ON FRIDAY ........ !!!! YOUNG DEE IN DA HOUSE....

..............."naitwa Arnie Gizzle........Unataka kujua leo nipo na nani humu ndani?"........... Ni moja ya maneno niliyokuwa najaribu kuzungumza kipindi nafungua show. Hapo kati nimeshatupia vitu zangu kutoka FELIX SINZA CLASSIC WEAR haajah jaah jaah!! nang'aa kama... Nway karibu katika show!!!!!!!!
Namwita bwana mdogo kiumri but mkubwa kwa jina, Anaitwa Young Dee!!! Hapa Gizzle na Crew ya Tupo Pamoja ilifanya kumtilia maguu kitaa na kuchonga nae Machache kuhusiana na Muziki wake na nini anafanya kwa sasa na pia tutegemee nini kutoka kwake?..... 
Unakumbuka ngoma ya Teacher?? iliyopikwa pale kati FishCrab na mtu mzima Lamar... This time Young Dee anakuja na project mpya kutoka Studio ya ukweli pale AUTHENTIC kwa mtu mzima MAX..... Daaaaah humo ndani kuna ngoma moja kali sana inaitwa KIATU....Daaah fanya kutazama show this Friday uwe wa kwanza kuisikiliza haaaaaa haaaaah!!!!!!
Huyu ndio Max wa AUTHENTIC ... Jamaa ni mkali wa sound na Idea kibao , zaidi ndio mtu anayempa training Young Dee kwa sasa pale kati... Pia ni msaani anayeimba ...... na anazo ngoma kibao na moja ya ngoma zitakazo make headline ni One Minute ambayo kafanya Collabo na Young Dee.... Fanya kucheck show afuu tuoneeeeeeeeee!!!!!! 
Huyu ni mchawi wa Beat anaitwa Erasto Mashine... Anapatikana pale kati AUTHENTIC ndio anafanya mambo yote mle ndani pia ndio mpishi wa track mpya ya Dee Inayotegemea kutoka hivi karibuni...... Unataka kumjua anafanyaje??? Don't miss the show @9pm this Friday Only on Ttv.
Baadae tukahamia pale kati pande za AEGS RECORD na hapa niki-show love na Nice P, Producer mkali hapa Bongo toka kitambo kwenye Game!! Moja ya Producers wanaofanya poa kwenye industry ya BongoFleva hapa Town. Nae alikuwa na machache ya kuzungumza humo ndani.... So Package imekamilika sana hapo kati.... Ukisikia Paaa usikose show...!!
Then Nilipiga Interview na msanii mkali kwa vocal RIZ NKANG'AA wa katikati ambaye hivi karibuni mtapata kuona Video yake mpya... Jamaa pia ni mkali toka kitambo bt alikuwa analisoma Game liko vipi...... Sasa anatisha sana kwani kashapata ramani ya kutoka!!! Unabishaaaaaah? Fanya kuona show then utaniambia..........!!!!!!!!!!
Hapo Nice P, pale Riz na hapa Arnie Gizzle tuki-show Love kwa pamoja... Huku nikiwa nimetupia vitu sumu kutoka pale FELIX SINZA CLASSIC WEAR pale SINZA- KIJUWENI haaah!!!! jaribu kufika pale Sinza afu tuoneee kama utatoka kavu!!!! Nway thnx kwa crew nzima ya TP, hapa nazungumzia Cameraman wangu Nurdin Msindo na David Langa, Make-up Annastazia Mairi (SADA), na Editor wa show the B.I.G Tommy (Thomas Mtefu

SO DON'T DARE TO MISS THE EXCLUSIVE SHOW THIS FRIDAY @9pm, REPEATED ON SUNDAY @8pm n' TUESDAY @5:30pm ONLY ON TUMAINI TV!!!!!!!!!!!!!!

Wednesday, September 29, 2010

USIFANYE KUKOSA HAPA ZONGHUA GARDEN THIS FRIDAY.


Ni official Video Launch ya "Sifai" kutoka kwa T.I.D na Top Band ft A.y na Lady Jay Dee this Friday pale kati bana . Si ya kukosa hii.....

VICHWA VINNE VIKALI NDANI YA UKISIKIA PAAA.


Unajua nini hawa jamaa ni noma sana katika suala la Hip Hop ebu chungulia hapa chini then utaniambia nini kinaendelea katika Industry hii........... Lyrics za Ukisikia PAAA,

Intro
ahhh...ahhhh
ohhh yeahhh..(shhhh!).. it's the remix
(shhhh!)...JCB....(ahhhh!).....Murder..!
(Tongwe Records Babyyyy)


Verse 1 (JCB)
Damu ilitapakaa baada ya ule mlio kulia PAAA,
Watu wote walisambaa hata walevi wa kwenye bar,

Sio polisi sio baunsa iliye kaa utashanga kwa nini mshkaji alizidi kumimina kwa kujiamini,
Amini usiamini akabaki tu na mimi,
Akanishikia bunduki kwa chini,
Akadai eti nimpe madini lasivyo ananipiga risasi kama sabini,
Anasura kama idi amini akarudi karibu atua tatu mpaka kabatini,
Akatamka HEYOO! nipo kazini nimetumwa mzigo au ujithamini,
Akanikanyaga kwa chini kikorofi bunduki tena akaikoki
Akasema kama simuonyeshi leo sio koki,jinsi alivyo akilenge ye akosi mikosi,
Kavaa koti jeusi jasusi,
Mikono nikaweka juu kuepuka nukx huku natukana mengi matusi...


Chorus X2
Ukisikia PAAAA...ujue imekukosa
Aliyelenga hana shabaha...amefanya makosa
Ukisikia PAAAA...ujue imekukosa
Aliyelenga hana shabaha...amefanya makosa


Verse 2 (Fid Q)
Wanasema hugeuka mnyama sana anaposaka pesa
Cha ajabu anavuta bangi lakini hawazii magangstar
Hampaki rangi donkey ili ageuke kuwa zebra
Ndo maana kabla hajaikoki, JCB ali-surrender
Akajifanya hayuko na mie ili niipigie defender
Nikaona vipi nijistukie ghafla nikasikia ''RASTA''
Jambazi linaniita halafu sioni wakuni-backup
Hali inatisha sikuongea nilishut the fluck up
Akaniuliza.. we sio Fid Q yule anayeheshimika mtaani ?
Nikamwambia ndo mimi na huu ndo muda wa kumlaani shetani
Sie wote ni watoto wa mjini siamini vipi hatujuani
Mie alwatani kama Kwere au Chindo popote amani
Akaniambia.. waambie machizi i'm sorry, leo mna-rap wapi ?
Mie sio mtu wa stories, i make things happen
Hii sanaa ni ya watengwa na ngosha...
Ukisikia Paaaaaaaa........ ujue imekukosa


Chorus X2
Ukisikia PAAAA...ujue imekukosa
Aliyelenga hana shabaha...amefanya makosa
Ukisikia PAAAA...ujue imekukosa
Aliyelenga hana shabaha...amefanya makosa


Verse 3 (Jay Moe)
(aahhh!) Alipogundua ni wasanii,haraka haraka akatuacha
Ndipo tulipomsihi,na watu wengine kuwaacha
Maana ishakuwa msala,na mashahidi nyuzi washavuta
So muda wowote defender,toka hivi sasa itafika
Bora usepe..kuliko kupewa kesi ya mauaji
Au kesi ya kujaribu,kupora kwa kutumia mkwaju
Hakuna mwenye mzigo,waambie wenzako mme-boogie
Na wala hatuna kimango,usione mezani kinywaji
Achana na mambo ya leo,wapi tunapiga show
Pigia wenzako simu,waambie huku ni soo
Hakuna mtu wa madini,sema ni kina jaymoe
Kabla haujaishia mikononi,kwa gorvo..au you know !
Ile anaanza kuchomoka tu,polisi washawasili
Nikasikia mikono juu..kwa sauti ya ukali
Kukimbia akala ya mguu,akasalimu amri
Akanyoosha mikono juu


Chorus X2
Ukisikia PAAAA...ujue imekukosa
Aliyelenga hana shabaha...amefanya makosa
Ukisikia PAAAA...ujue imekukosa
Aliyelenga hana shabaha...amefanya makosaVerse 4 (Chidi Benz)
Hata police ni mdili na ndo mchongo ameupanga..
Na ndo yeye wamemtuma jukumu lake kuwa mwanga...
na ile paaahh!! Kama Suka kama kulenga mchanga
Mwisho wa siku mahesabu watu wakacheze fanga
Mchezo kamili ulishapangwa yaliyopita ni historia...
na maneno kaa ya kwenye kanga ya hesabu nishatulia
Wa kucheka wamecheka wa kulia wamelia
Nchi bado haikufea so hamtochoka kusikia
Michezo kama hii kurudia ninajua walala hoi
Wamechoka vumilia...yeeahh
Damu zitamwagika kwa wema na wasio wema...
na imani ya mkabaji ulichokimeza utakitema
Kuna movie ila maisha ka cinema
Unyang'anyi na uchukuzi unaoatokeo kila nikihema ...(hema)
Wanasema ukila nyama....lazima utake tena..
na kweli macho kwa maneno ya viongozi wanaosema
Ni vigumu kutumkia kabla tonge kuingia
So anytime tuwe tayari kuumia....yeeahh
Ni vigumu kutumkia kabla tonge kuingia
So anytime tuwe tayari kuumia....yeeahh


Chorus X2
Ukisikia PAAAA...ujue imekukosa
Aliyelenga hana shabaha...amefanya makosa
Ukisikia PAAAA...ujue imekukosa
Aliyelenga hana shabaha...amefanya makosaHilo ndio goma la ukweli kwa kufungia mwaka huu wa 2010 kwa wana-Hip Hop wa ukweli .. Fanya kuutafuta wimbo huu!!.

Monday, September 27, 2010

Friday, September 24, 2010

TUPO PAMOJA SEASON II IS BACK. USIKOSE LEO SAA 3 USIKU ONLY ON TUMAINI TV.

The returning of Tupo Pamoja Season II.... hope unakumbuka ile show kali na ya kijanja Town with ur Boy Arnie gizzle now is back as usual baada ya mapumziko ya muda mrefu... this time inakuja kivingine kabisa so don't miss it... Full Swagger na macelebrity wanayoiweka industry ya Bongo fleva on Top in Town.......

This week Crew nzima ya TP ilitia timu pale kati ya magomeni na kukutana na wamiliki wa Umabe Co. ndani ya RAMA RECORDS.. Mengi sana yalitupiwa humo ndani ....

Victor Mrisho a.k.a Kita ni moja ya member wa UMABE Co. pia ni bonge moja la Producer pale Rama Records ambaye hivi karibuni atatishaaaaaaa vibaya sana , kwani ana uwezo wa kunyonga Beats na ku-blaze hits maaaaaaaaaama!! ni sooooo mpk kupata jointventure na wana toka Obamaland ambao wanaanza kutia maguu Bongo kuanzia Jan 2011 kwenye bonge moja ya Project!!!!!! zaidi ni mkali wa mashairi ......Fanya kuchungulia show Ijumaa ya leo saa 3 usiku afu tuoneeeeeeeh!!!

Wengi mnamfahamu kama Azma Mponda former Prime Minister wa IFM na founder wa UMABE Co..... pale kati ktk studio ya Rama Records akitupia vocal... yumo ndani ya show na mating'aa yote ya kutosha....... TP Only on Ttv

Dogo wa kwanza kushoto anaitwa Porrigde ni mkali wa ku-Rap ile mbaya ... then nilikutana nae pale Studio akimaliza kuingiza Vocal zake nakutupia yake kuhusu Industry yetu kwa ujumla toka kitambo mpk sasa..... Hapo wakiwa wametinga mat-shirt ya UMABE production........


Daah Show imesimamiwa na mtu mzima Arnie Gizzle, Cameraman Samson Tibba (The General) na kufanyiwa maujanja ya kutosha na mtu mzima Thoms Mtefu (Big Tomy),, Ukisikia PAAAAH ni noma nikiwa nimetupia vitu vikali sana kutoka pale FELIX SINZA CLASSIC WEAR...... For allstars pale kati Sinza kijiweni.....ukitaka kuonekana Nadhifu fika hapo kati afu tuone.


DON'T DARE TO MISS THE SHOW THIS FRIDAY N' EVERY FRIDAY @9PM ONLY ON Ttv!!
HAPPY BIRTHDAY MH. ZITTO.

Mdau leo tar 24 Sept ni siku ya kuzaliwa kwa mmoja kati ya wanasiasa Vijana na wakali nnaowaaminia nchini Nchini Tanzania Zitto Kabwe... so Mh. huyu anasheherekea siku yake leo huku akiwa katika kampeni kali ya ku-support Kijana mwenzake anegombea jimbo la Ubungo Bw. John Manyika.... kama nawe ni B'day yako leo fahamu kuwa unashea b'day na Mwanasiasa huyu...Happy B'day Zitto Kabwe n' All the Best!!

Tuesday, September 21, 2010

MWISHO NA SHEM NDANI YA JACUZZI (BBA ALL STAR).


After the Nominations show, washindi walioingia Top five wakatupia nguo kuleeeee then shaap dip in the jacuzzi. But daaaaah Bro Mwisho na shem wa Tanzania (Meryl) walipiga bonge bonge moja la deeeeeeeeEEEEeeep KISS almost four minutes .... daaaaaah ilikuwa utata pale kati mzeee!!!!.

Wadau tufanye uzalendo Bro wetu arudi home na kitita cha madollar kwa kumuokoa kutoka mjengoni by voting thru www.mnetafrica.com/bigbrother then utakuta maelekezo how to vote or thru ur mobile phone.

VOTE 4 MWISHO VOTE 4 TANZANIA.......!!!!!!!!!!!!!!!!

Monday, September 20, 2010

MUSIC LAB YAWATANGAZIA OFFER BAAB KUBWA MA-UNDERGROUND WOTE WA BONGO.KWA WALE WASANII WACHANGA AMBAO WANAJIONA WANAKIPAJI LAKINI WAMESHINDWA KUTOKA,SASA DAWA YAO IMEPATIKANA KUTOKA KWA PRODUCER WA UKWELI ASIYEKUWA NA LONGOLONGO DUKE TACHEZ,AMBAYE AMEWEZA KUTENGENEZA NGOMA KIBAO KAMA I'M PROFFESION YA FID Q,PLAY BOY YA NIKKI MBISHI,INCREDIBLE YA ONE NA NYINGINE KIBAO,NAFASI IMEPATIKANA SASA CHANGAMKIENI OFA HII........

STUDIO HII YA MUSIC LAB( M-LAB) IKO ENEO LA KINONDONI KARIBU NA UWANJA WA BIAFRA KWA MAWASILIANO ZAIDI MTUMIE EMAIL duketachez@hotmail.com AU PIGA SIMU NO 0714 884342


KWA hisani ya www.nyanjap.blogspot.com

HAPPY BIRTHDAY DJ CHOKA.

Haaaaaaaaaaaaaaaaa bro mkubwa niaje aje bana? jana pande za pale kati Mzalendo pub watu tulikula keki kwa sana...... So ndio miaka mingapi sasa?
Nway mtu mzima nakutakia maisha marefu kwa pamoja tuendeleze libeneke ili hapa Bongo mpk Next level ndg.........................ALL THE BEST BRADA!!!!!!!!!!!!!!!!

Saturday, September 18, 2010

TUSKER PROJECT FAME IN TANZANIA.......

Hii ni kutoka East African Breweries Ltd. Ambapo leo wanapiga bonge moja la Audition hapa Peacock Hotel (Dsm) kwa aili ya kupata washiriki for the fourth season of Tusker Project Fame (TPF).
Nimekutana na vipaji kibao hapa nje na wakiwa wanajiandaa kwenda kufanya usahili huo ambapo kwa wenzetu Rwanda na Kenya wameshamaliza Auditions zao.

The competition is open kwa wana-East Africa wote above 21 years of age, wenye uwezo wa kuimba, compose na ku-play any musical instrument. Washindi watafunguka na superstar titles, huge cash and record deals with South Africa’s Gallo records.

2010 itakuwa wiki 8 ya reality show ambazo zitaongozwa na some of the region’s great hosts and MCs – Gaetano Jjuko Kaggwa, and MC Mitch Egwanga.

In 2009, Rwanda’s Alpha Rwirangira, 24, alifunguka na Ksh5 million, a one-year deal with South Africa’s Gallo Records company and Premier Plus Medical cover from Resolution Health among the many prizes.

Wednesday, September 15, 2010

DR. O ANAENDELEZA HARAKATI A-TOWN.... HIP HOP MOVEMENT.

Kama askari anavyoiwakilisha Bongo, na A-Town inasimamishwa na hicho kitu mbele yako......... Mkali wa Rhymes of All Time Michael Yongo ama Dr. O yupo pande hizo akiendeleza Movement za Hip HOP......
Hapa alipokutana na mkali Jcb Makalla Mtengwa anayeiwakilisha Arusha kwa sana as they say Hip Hop ndipo ilipozaliwa .......
Katika pozi ... Thru  facebook chat nilimuliza swali na zaidi nikamwambia mbona shavu??? daaah kanitupia mistari hatari ebuuuu pitia na wewe daaaaah.....  "Arniegizzle mashahiri yamejaa kichwan, mpaka natoka shavu, ni mbabe wa kugani, japo sina mbavu, 2ngo zangu angavu ndo zinawafunza wapumbavu, kipindi ni 2po pamoja zingene kavu, utanikuta ijumaa nakipimia laivu. bigup kwa wote wanaosupport mvmnt".... Daaah untishaaaaa mwanajeshi wangu!!!!

Unaweza mcheki pia kwenye:- www.doctoryongo.blogspot.com

Tuesday, September 14, 2010

HAMIDU KUGAWA BURE ALBAMU YAKE YA SIKATI TAMAA.

New album ya Hamidu sasa inapatikana na haiuzwi jamaa ameamua kuigawa, so kama unaitaka na upo pande za Dar es salaam basi jaribu kupitia maeneo ya Kinondoni Studio kwenye duka lake la nguo halafu mpango mzima utaupata hapo. Kwa wale mafans wake wa mikoani kuweni na subra jamaa atatoa utaratibu soon!!!!!!


kwa hisani ya djchoka.blogspot.com

LADY GAGA NA VAZI LA NYAMA KWENYE STAGE YA MTV's VMA!!!!!!!!!!!

"I never thought I'd be asking Cher to hold my meat purse." Ni moja Gaga's unusual statement alipo-step kwa stage ya MTV's Video Music Awards on Sunday kuchukua Her Video of the Year Award kutoka kwa Legend wa Pop Cher...

Huyu ni mwanadada mchachari mwenye fans wengi ulimwenguni kutokana na vituko vyake...... Lady Gaga alitupia hapo kati vazi la nyama (plus boots, hat n' purse) kutoka kwa mbunifu wa mavazi Franc Fernandez......
Mpk leo huyu Gaga anatisha kwa mbwembwe zake kitu kinachomfanya kujinyakulia mashabiki kila kona ya Dunia....................... Daaaaaaaaaah all Eyez on Her!!!!!!!!

Monday, September 13, 2010

THE FIRST LADY WA TIP TOP KAJITOA KUNDINI.

Ni khadija Shabaani the fist lady wa Tip Top Connection ambaye kwa sasa ameamua kujitoa kundini kwa madai ya maslahi madogo .... na hizo ni Habari zilizopo mtaani kuhusiana na Keisha ku"mind" Manager wa kundi hilo Babu Tale kuwa anamdai dough kibao za show na vitu kama hizooooooo......

Akidhibitisha ilo Leo ktk XXL ya Clouds fm Babu tale amesema " Keisha kaomba kupumzika na sisi tumeamua kumpumzisha milele"....... Mpk hapo ukweli upo mikononi mwa wahusika ......
Wasanii kibao wa Bongo wamepitia Tip Top Connection na kila wakitoka wanalalamikia masilahi, But still kuna wakongwe wa miaka nenda Rudi...... mpk leo hakijaeleweka kunani pale??????????

Wednesday, September 8, 2010

SO PWAA (PWAA PART III) NI TETEMEKO LA MJI..............

Balaaaaaaaaaaaaaaa kwani ni Bonge bonge moja la clunk of all time Produced by Lucci ,Vocal & Mixing by Lamar wa Fishcrub...... Na Bonge bonge moja la Video kutoka kwa bro Adam Juma wa Visual lab "Next Level"....... Nazungumzia SO PWAA (Pwaa part 111)..........

All over Town ni gumzo ya So Pwaa.... Media almost zote za burudani ni So Pwaa... Yaani He gotta Lucci on the Beat, Lamar blaze the Hit......................... nani anasema Bongo fleva inakufa? wanaofilia mbali ni ma-weak Mc's............... so pwaa get on floor, get on floor n' c how low can u go????????? moja ya mistari iliyonipa mzuka pale kati pwaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!
Ndani ya Video utakuta KIDUKU kwa kwenda mbele,,,, swagger za kutosha toka kwa vijana wa THT, Babuu wa Kitaa, Fid Q, Lamar, Rommy Jones, Lucci na flowers wa kutosha sana............ ni so kama ilivyo so pwaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!! Watch out on ur TV!!!!

TATTOO ZA RIHANNA ZAWA GUMZO...

The "Good Girl Gone Bad" singer akiwa katika muonekano wa faux tattoos, including a pistol kwenye paja lake. Hapo mwanadada alikuwa akila bata kwenye ufukwe wa Hawaii baada ya kazi ndefu ya film ya "Battleship".

Wadau si urembo, hiyo ni kwa ajili ya movie anayofanya bana so.....................................

BONGE BONGE MOJA LA NOMINATION CELEBRATION PARTY...

Pale kati unatupia then unakuja ku-party na ma-celebrity kibao wa bongo kumpa shavu mwanadafada Witnesz ........ Uwepo wako ni support tosha kui-push Tanzania to the Next Level.......!!!!!!!

Monday, September 6, 2010

BAAAAAAAAAB KUBWA NI FRIENDS CONNECT ZONE!!!!!!!!!!!!!!!!!

Kwanza pole na kazi zako zote za kila siku na asante kuendelea kutupa burudani taarifa za papo kwa hapo kila wakati tunapo hitaji, umetufikia mpaka huku machimboni.


TOVUTI MPYA YA FRIENDS CONNECT ZONE
Nilikua naomba unisaidie kunitambulishia tovuti yangu ambayo ni mpya kabisa machoni kwa watu wote mimi ni mtanzania. Baada ya kukaa chini na kufikilia nimeona nije na wazo jipya la kuanzisha tovuti ambayo itawakutanisha watanzania mbali mbali na watu mbali mbali popote Duniani, kwa lugha ya kigeni tunaita Social Network.

Katika tovuti hii ya Friends Connect Zone. ni rahisi sana kutumia na pia kujiunga, pia mtumiaji anaweza jiunga kupitia Facebook ama myspace mtumiaji akiwa ndani ya tovuti hii ataweza tafuta marafiki,ataweza weka picha zake,video,blogs na mambo mengine mengi.


Si hivyo tuu mtandao huu mpya utakuwezesha kuchat muda wote ambao atakuwa hewani na marafiki watakao kuwa hewani,pia ataweza kuona yuko wapi katika muda wa nchi aliyopo.Nawaombeni ndugu zangu tujiunge katika mtandao huu, na pia tuwaalike na wenzetu wapate kujiunga, kwa pamoja tuendeleze tecknolojia nchini kwetu,na mawasiliano kwa ujumla, nawashukuruni nyote na karibuni sana.


Jina la website: Friends Connect Zone


Link ni: http://www.friendsconnectzone.tk/


email:friendsconnectszone@gmail.com


Natanguliza shukurani zangu.....

KANYE WEST BADO ANAJUTIA ALICHOMFANYIA SWIFT LAST YEAR.

Mtu mzima Kanye West alipovamia stage na kumpokonya Mic mwanadada Taylor Swift mwaka jana kwenye Tunzo za MTV........... Leo hii anajutia sana

Hip-hop star Kanye West bado anafeel the pain kutokana na ambush aliyofanya mwaka jana kwa mwanadada Taylor Swift. Ame-express his pain kupitia mtandao wa Twitter this Saturday.
Kanye amekili kwa mara nyingine kuwa alifanya kosa kwa kurukia on stage na kumpokonya microphone Swift na kutamka kuwa hiyo Trophy anastahili aipate Beyonce na sio yeye kwenye tamasha la MTV Video Music Awards..

Kanye ka-apologize tena kwa Swift na kusema amemwandikia song kwa ajili yake na anamatumaini she will perform..... "kama asipouchukua nita-perform kwa ajili yake," he said..

West kwa sasa ana-work on his new album ambayo inategemea kutoka sometime this fall. .

Thursday, September 2, 2010

WADAU WA MITANDAO JIHADHARINI NA MATAPELI KAMA HAWA.

wadau nilikuwa nipo kidogo na jiji kwa masuala fulani ya kiofisi mkoani Iringa yalipo makao makuu ya Ofisi yangu Ebony Fm..... So u-busy mwingi ukanifanya niwe mbali kidogo na computer na mambo mengine kama hayo. watu wangu wa Iringa, Mbeya na wote wa Nyanda za juu kusini hope mnatambua nini MTIKISIKO??? Bonge moja ya event pande hizo....... inayoni-keep busy sana

Nway baada ya kufungua E-mail yangu leo asubuhi nikakuta E-mail kibao sana zikiwemo za kiofisi na mambo ka hayo but nilishutuka sana kuona hii mail hapo Down.. nilipoisoma ikanibidi niwashilikishe na wadau jinsi watu wanavyotumia mbinu nyingine kutapeli.. tuweni makini na watu kama hawa jamani..

Soma kwa makiniThu, September 2, 2010 5:29:05 PMFBI...UNDER INVESTIGATION
From: INVESTIGATION DEPARTMENT


--------------------------------------------------------------------------------

Anti-Terrorist and Monitory Crimes Division.
Federal Bureau Of Investigation.
J. Edgar. Hoover Building Washington D.C

Attn: BENEFICIARY
This is to Officially Inform you that it has come to our notice and we have thoroughly Investigated by the help of our Intelligence Monitoring Network System that you are having a Legal Transaction with the Federal Ministry Of Finance Nigeria. During our Investigation, it came to our notice that the reason why you have not received your payment is because you have not fulfill your Financial Obligation giving to you in respect of your Contract/Inheritance Payment.
And we have been notified that you are been contacted by the non-official who are trying to divert your fund, stop contact with any other office and deal directly with this office;as we have also having records with other people you have been dealing with.
So therefore, we have contacted the Federal Ministry Of Finance on your behalf and they have brought a solution to your problem by arranging your payment in total of US$4,600.000,00 as been part payment in an ATM CARD which you will use to withdraw money in anywhere of the world.or DIRECT WIRE TRANSFER into your account You now have the lawful right to claim your fund in the ATM CARD by contacting the ATM CARD CENTER or submit the following details for the onward transfer of your fund via the wire transfer mode:
*A scanned copy of your identity.
*Contact telephone/Fax number.
*Contact address
*Your banking details
You are to contact at this office within three working days for the time you have received this email .
God Bless America.

FBI Director
Robert S. Mueller