Thursday, August 26, 2010

TIP TOP CONNECTION WAKAMILISHA ALBAMU YAO..

Kundi linalo-make headline hapa bongo kutoka Manzese, Tip Top Connection wamaliza Albamu yao ya pamoja itakayokwenda kwa jina la TUNAPANDA yenye jumla ya majisong 14..

Ni Albamu ambayo wameamua kuifanya ya kiAfrika mashariki sana huku wakiwa wamefanya kollabo na wasanii wa ukanda huu wa Afrika Mashariki, Kutoka Kenya mzee mzima Nonini kawakilisha, Uganda wakasimama na Michael Rose na hapa Bongo kasimama A.Y pamoja na kundi matata la TMK Wanaume!!! Bonge la Albamu huku likiwa limetupiwa mikono kutoka kwa maproducer tofauti tofauti kama Enrico wa Soundcraft, Macko chali wa Mj Record, na Pancho wa B.Hits..!!!!!!!!!!!
Hayo yamesemwa na kiongozi wa kundi hilo Rais wa Manzese Madee kupitia kipindi cha XXL ya Cluods Fm kupitia segment ya 255 (2 gwafala gwafala) na Ncha kali....... Zaidi wanategemea ku-Lauch siku ya Eid-Mosi. Tip Top Connection na TMK Wanaume ni moja ya makundi yenye mfano mzuri wa kuigwa kwa ushirikiano wao... Kila la kheri wana!!!!!!!!!! 

No comments:

Post a Comment