Wednesday, August 18, 2010

DEAR MAMA........ HASHEEM THABEET.

Uchungu wa mwana aujuae mzazi, hilo ni neno la kiswahili linalobeba maana sana. Hayo yamethibitishwa na Mama mzazi wa mchezaji nyota wa Tz anaecheza ligi ya NBA -timu ya Memphis Grizzlies Hasheem Thabeet (7.3ft) , alipofanya bonge la Interview na Dina Marios kupitia kipindi cha Leo Tena ya Clouds fm........ Mama Hasheem kajaribu kuelezea maisha yao kwa ujumla wapi walipotoka mpk sasa walipo... Zaidi kaelezea msoto aliokula na wanae baada ya Mme wake kukatika mwaka ya 2004...

Amesema pamoja ya msoto huo, pia alikumbana na kero kibao pale alipokuwa anapita kitaa na Mwanae then watu wanamcheka kutokana na urefu wa dogo kwa kumwita majina ya kejeli , wengine wakidiliki kumfananisha na jini mtu kitendo ambacho kilimsononesha sana Bi mkubwa .. Bi mkubwa anadai tabu nyingine aliyopata ni pale viatu vya Dogo vilipohitajika daaaaaaah !!! bila kwenda mtumbani huwezi pata dukani kutokana na urefu wa mguu wake, then jamaa walikuwa wanampiga bei mbaya kutokana na design hizo kuwa Adimu hivi....
Bi mkubwa kaelezea mengi kuhusu maisha ya familia yake hili kwa sasa anamshukuru sana Mungu kwani sasa anakula Bata MreFFFfffffff.............. kwa kwenda mbele kwani dogo ana-appreciate Bi mkubwa alivyo-husttle kuwafikisha walipo baada ya Dingi kukatika. Kilichonifurahisha ni pale Dina alipomuliza swali la kizushi kuwa ni kituko gani Hasheem alishafanya ambacho Bi mkubwa hawezi sahau................................ Daaaaah kumbe kipindi yupo school jamaa alikuwa bonge la mtemi, nunda au mbabe mbaya!!! alikuwa anapiga biti mdogo wenzake wamletee mkwaja wa kula shule la sivyo wasitie maguu skongaaaaaaaaaaaa otherwise wanachezea kichapo...... haaaaa hah ha hah ha!!!!!!!!!!!
Big up Mwana umetuonyesha njia kuwa everything is possible nikuongeza bidii tu!!!!

No comments:

Post a Comment