Friday, July 23, 2010

WAGOSI WA KAYA WAMEGUKA.....!!!!!!!!!!!

Kutoka jijini Tanga Shetani muaji wa makundi katembelea kundi la wagosi wa kaya, hayo yamedhibitisha na member wa kundi hilo John Simba "Dr. John" ambaye amedai kuwa kufa kwa kundi hilo ni kutokana na mwenzake Fredy Maliki "Mkoloni" kujiingiza ktk masuala ya kisiasa.

Dr. John anasema kutokana na Mkoloni kujiunga chama cha Chadema, hivyo kila kitu ambacho kitakuwa kinafanyika ndani ya kundi hilo kama kuimba na mengine itakuwa maagizo ya Chadema.

Aidha Dr. John amesisitiza kuwa kwa sasa anataka kufanya kazi peke yake kama solo Artist kwa kushirikiana na wasanii wengine hapa Bongo, lakini kizuri zaidi ni kuwa urafiki wao na Mkoloni utaendelea kubaki pale pale kama zamani hila utofauti utakuwa kwenye kazi tu......

Habari kwa hisani ya www.ankomo.blogspot.com

No comments:

Post a Comment