Thursday, July 1, 2010

MWANA HARAKATI KAMA Mr. 2 a.k.a SUGU ANAPOAMUA KUGOMBEA UBUNGE!!!


Mwana-Harakati na Mkongwe wa Hip Hop Tanzania,Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu ametangaza nia yake ya kugombea Ubunge kwa tiketi ya CHADEMA, jimbo la Mbeya mjini.

Mheshimiwa mtarajiwa yuko Mkoani Mbeya akiwa kwenye mchakato wa kurudisha fomu baada ya kupata ridhaa ya chama chake...Mr. 2 au Sugu anaungana na wasanii wengine toka Tanzania kama Kalama Masoud a.k.a Kalapina anatakayegombea Udiwani jimbo la Kinondoni-DSM kupitia chama cha CUF na Nakaaya Sumary aliyetangaza nia ya kugombea Ubunge mkoani Arusha kwa tiketi ya CHADEMA... Daaaaaah!! huu ni mfano wa kuigwa kwa wasanii hawa wa muziki wa Hip Hop nchini.. Na ukisikiliza ngoma zao kwa makini utasikia wanazungumzia mambo ya kijamii indeep......! so waheshimiwa kila la kheri 2010.....    Sourcempangomzima.blogspot.com 

No comments:

Post a Comment