Friday, July 9, 2010

MTU PEKEE NI WEWE..................!!!!!!!!!!

Ni mida ya saa 4 na dakika kadhaa usiku natokea kazini kuelekea Home, nikiwa barabara ya Morogoro ( mataa ya njia panda ya Moro road na Bibi titi road). Naona kwa mbali kundi la watoto kama wanne wameinamia kitu. Taa nyekundu ikawaka na gari ikasimama, nilimwomba dereva aweke gari pembeni, nikashuka kujua ni kitu gani wanafanya usiku huo? Ni watoto ambao wameshakata tamaa na maisha na hawana matumaini na kesho... "hoyaaaa braza unasemaje au we mnoko?" Sauti ya uchovu kutoka kwa mvulana mdogo makamu ya miaka 11-13 hivi akiniulizia nini nataka.

Kabla sijajibu lolote nilijiuliza maswali mengi sana..................... Ilinichukua muda kunikubalia kuzungumza nao. Mwishowe tulizungumza mengi sana na nikagundua kuna sababu nyigi sana zinazo wapelekea kuchagua kuishi maisha ya mtaani kuliko maisha ya kawaida ya kifamilia. Chanzo cha yote hayo upelekea watoto hawa kuishi katika mazingira magumu kujaribu kutafuta fedha kwa kwa kazi za watu kama kubeba mizigo, kuuza maji na biashara ndogo ndogo pamoja na kuosha magari n.k. wakati wa usiku ulala popote wanapoweza na nzuri zaidi waliniambia ushirikiana kwa kila wanachokipata , hula pamoja na kusaidiana kwa mambo mbalimbali.........................

Kwa muda huo nilishindwa kufanya chochote, nilirudi kwa gari ninam majonzi makubwa kwa stori nilizotoa kwa watoto hao. lakini nilipofika Home nilitafakari sana kuhusu watoto wa mitaani na hasa hawa wanaotumikishwa mitaani. Nikaona watoto hawa wanahitaji mtu kusimama kwa niaba yao na kuwa msemaji wao. Na mtu pekee ni MIMI- kama mzazi, mwandishi wa habari na mtu mzima ambaye naona ukiukwaji wa haki za watoto...........................

Wewe na Mimi tukishikamana tunaweza kupinga utumikishwaji wa watoto na kuwapa haki zao na kuifanya Tanzania inayofaa watoto kwani Tanzania inayotufaa sisi, humfaa kila mmoja. Zaidi tembelea hii web: www.stopchildlabour.eu . Ni kusupport kampaini ya kupinga utumikishwaji wa watoto na kuhakiki watoto wote duniani wanakwenda shule...........

No comments:

Post a Comment