Friday, July 23, 2010

WAGOSI WA KAYA WAMEGUKA.....!!!!!!!!!!!

Kutoka jijini Tanga Shetani muaji wa makundi katembelea kundi la wagosi wa kaya, hayo yamedhibitisha na member wa kundi hilo John Simba "Dr. John" ambaye amedai kuwa kufa kwa kundi hilo ni kutokana na mwenzake Fredy Maliki "Mkoloni" kujiingiza ktk masuala ya kisiasa.

Dr. John anasema kutokana na Mkoloni kujiunga chama cha Chadema, hivyo kila kitu ambacho kitakuwa kinafanyika ndani ya kundi hilo kama kuimba na mengine itakuwa maagizo ya Chadema.

Aidha Dr. John amesisitiza kuwa kwa sasa anataka kufanya kazi peke yake kama solo Artist kwa kushirikiana na wasanii wengine hapa Bongo, lakini kizuri zaidi ni kuwa urafiki wao na Mkoloni utaendelea kubaki pale pale kama zamani hila utofauti utakuwa kwenye kazi tu......

Habari kwa hisani ya www.ankomo.blogspot.com

Wednesday, July 21, 2010

DOGGY 'S BACK, WELCOME BACK HOMMIE..

Kama time za asbh ya leo mida ya saa 1 moja hivi pale Mwl. Nyerere International Airport mwana kashuka baada ya bata mrefuuuuuuuuuu wa takribani 3 weeks hivi katika miji tofauti tofauti za U.K....................... Kila kitu kimeenda poa sana na show zote zilisimama kwa sana.... Mb Doggy anatoa shukrani kwa funs wote walio-show love pande hizo!!!!!!!!! WELCOME BACK HOMMIE!!!!!!!!!!!...... Tulikumiss sana!!!!!

Friday, July 16, 2010

WEEK-END NJEMA WADAUU!!!!!!!!!! BATAAAAAAAAA

Kila mwisho wa wk hasa "FURAHI-DAY" wengi upendelea kutoka mitoko tofautitofauti.... kula bata za hapa na pale hili mradi kuweka akili sawa Baada ya miangahiko ya wiki nzima............... so nawatakia Bata mwema but iwe kiasiiiiiiiiiiiiiiiiii........... HAPPY FRIDAY!!!!!!!!!!!!!

TALK OF THE TOWN ALL TIME.........

Hii haijawahi tokea katika Historia ya Muziki hapa Bongo..... Daaaaaaaaaaahh inanikumbusha henzi za 2pac na B.i.g kitu cha "Hit im up" ambacho kilisambazwa kwa njia ya net na kikaspread kwa haraka zaidi....................
Tofauti na Anti-Virus Mixtape Volume-1, Siwezi ita beef hila ni Hip Hop... unaweza elewa namanisha nini hila ni hisia na mtazamo wa wasanii hawa juu Industry ya Music Hapa Bonge.
Haijawai tokea ... wanajiita VINEGA. Daaaaaaaaahhhhh ni TALK OF THE TOWN!!!!!!!!! Fanya kuitafuta then utakuja na lakwako ikishaisikia....

UKWELI KUHUSU NGOMA MPYA YA KIDUMU NA JAY DEE (NITAFANYA)..

KUTOKA KWA HERMY B.......
Kidum alipokuja Dar aliamua kumtafuta Hermy B ambae alikutana nae Project FAME kule Nairobi.Wakakutana na kufanya kazi pamoja..katika maana ya kwamba muziki huu uliundwa na Hermy na Kidumu akitoa melodies. Drum Patern Yote ni Ya hermy. Kidum aliporudi kule Nairobi akakutana na Rkay(jamaa anaetengeneza mziki wa Wahu examples Sweetlove, Runin Low) madhumuni ni kutengeneza video ya wimbo huu.Cha ajabu Rkay akamtengeneza Kidum mpaka akakubali kurekodi upyaa wimbo huo.
Rkay alikopi kila kitu ila akabadili sauti tofauti kidooogo, ila kisheria alibeba Idea ya kisanii ya Hermy kama ilivo. yote haya yalifanyika bila kuomba ruhusa wala kumpa taarifa Hermy.Muda ulipofika Hermy alitoa huo muziki kwa radio stesheni, na kidumu alikimbilia kuomba wasiucheze huo wasubiri ule wa Rkay..alipoulizwa huu una tatizo lipi alishindwa kujieleza na akagundulika hana mantiki zaidi ya Ubaguzi wa sanaa tu. Stesheni flani flani wakakubali kuupokea na kuucheza huu wa kwetu Tanzania.
Hermy hakutaka kuongea chochote kile mpaka alipoona wimbo huo wa Rkay ukichezwa na upo kwa video aliyopiga Rkay kwa sasa.Mwenye maskio na aliyeskia wimbo huu mara ya kwanza atajua tu huu uliopo kwenye video ni tofauti na vyombo vimepunguzwa, sio kwamba Rkay hajui kutengeneza muziki, ila alikua akijaribu kujitofautisha sana na Hermy na amejikuta akiharibu kiasi flani sanaa hiyo.
Ninachoomba ni kwamba watanzania tuendelee kushikamana na kupeana suport kwenye wizi wa sanaa kama huu. Tuwe na cha kujivunia kwa watengeneza mziki wetu. Asalaamu!
Kwa hisani ya http://www.djchoka.blogspot.com/

Friday, July 9, 2010

MTU PEKEE NI WEWE..................!!!!!!!!!!

Ni mida ya saa 4 na dakika kadhaa usiku natokea kazini kuelekea Home, nikiwa barabara ya Morogoro ( mataa ya njia panda ya Moro road na Bibi titi road). Naona kwa mbali kundi la watoto kama wanne wameinamia kitu. Taa nyekundu ikawaka na gari ikasimama, nilimwomba dereva aweke gari pembeni, nikashuka kujua ni kitu gani wanafanya usiku huo? Ni watoto ambao wameshakata tamaa na maisha na hawana matumaini na kesho... "hoyaaaa braza unasemaje au we mnoko?" Sauti ya uchovu kutoka kwa mvulana mdogo makamu ya miaka 11-13 hivi akiniulizia nini nataka.

Kabla sijajibu lolote nilijiuliza maswali mengi sana..................... Ilinichukua muda kunikubalia kuzungumza nao. Mwishowe tulizungumza mengi sana na nikagundua kuna sababu nyigi sana zinazo wapelekea kuchagua kuishi maisha ya mtaani kuliko maisha ya kawaida ya kifamilia. Chanzo cha yote hayo upelekea watoto hawa kuishi katika mazingira magumu kujaribu kutafuta fedha kwa kwa kazi za watu kama kubeba mizigo, kuuza maji na biashara ndogo ndogo pamoja na kuosha magari n.k. wakati wa usiku ulala popote wanapoweza na nzuri zaidi waliniambia ushirikiana kwa kila wanachokipata , hula pamoja na kusaidiana kwa mambo mbalimbali.........................

Kwa muda huo nilishindwa kufanya chochote, nilirudi kwa gari ninam majonzi makubwa kwa stori nilizotoa kwa watoto hao. lakini nilipofika Home nilitafakari sana kuhusu watoto wa mitaani na hasa hawa wanaotumikishwa mitaani. Nikaona watoto hawa wanahitaji mtu kusimama kwa niaba yao na kuwa msemaji wao. Na mtu pekee ni MIMI- kama mzazi, mwandishi wa habari na mtu mzima ambaye naona ukiukwaji wa haki za watoto...........................

Wewe na Mimi tukishikamana tunaweza kupinga utumikishwaji wa watoto na kuwapa haki zao na kuifanya Tanzania inayofaa watoto kwani Tanzania inayotufaa sisi, humfaa kila mmoja. Zaidi tembelea hii web: www.stopchildlabour.eu . Ni kusupport kampaini ya kupinga utumikishwaji wa watoto na kuhakiki watoto wote duniani wanakwenda shule...........

Tuesday, July 6, 2010

KITU CHA MKESHA WA SABASABA (7 7)............

Pale kati Jay Dee na Machozi Band + Dj BoniLuv & Dj Mackay ... itakuwa freshhhhhhhhhhhhh pale Mzalendo Pub leo terehe 06/07/2010...... daaaaaaaaaaaaaag Si ya kukosa hii wana Das'lamu na vitongoji vyake........... PAAAAH!!TUKUTANE PALE KATI!!!!!!!!!!!!!!!!!

Friday, July 2, 2010

HII NI ZAIDI YA FID Q.COM....... CHEUSI DAWA............

"Nilianza rap kabla mototo wa Dandu hajafu, Sugu hajatoa Album, BoneLove hamjui Falsafa mlangoni msanii analipa, Professer anajiita Nigga’".......... Fid Q AU Ngosha Ze Swagga Don ama Cheusi Dawa kama anavyojulikana ktk Hip Hop Industry hapa Bongo..... Namfeel sana huyu mwana kuanzia swagga zake na hasa lyrics zake zilizoenda shule.....
Now hii ni kwa wale mafans wanaotaka kumjua Fareed Kubanda kwa undani zaidi kuhusu maisha yake binafsi na hata kazi zake za kimuziki fanya kutembelea www.cheusidawa.blogspot.com ....na mwisho kwa wadau "if you passionate about Hip Hop try listening to His songs"............................................ 1 LOVE.

Thursday, July 1, 2010

MB DOGG ALIVYOSWAGISHA NDANI YA MJI WA MILTON KEYNES.....

Kama kawa brada wa Malov dav kwa kuimba kwa hisia ndo zake..... mwanzo mwisho Dogg...........
Can u Imagne unaenda mbele na kukuta mafans kibao hao ...... Daaaaaag! kumbe Mbele ka cha home watu busy kuchukua pix kwa 4ne!!!!!! nilidhani Bongo tuuuuuuu
Kama namsikia alikuwa akiimba ngoma gani???????? Unabishaaaaaa hicho kitu cha Saga Plasher..........
Big up mwana .................. U.K 1 LOVE.... Ukirudi lazima nikudake 2pige show pamoko ndani ya Tupo Pamoja.....

MWANA HARAKATI KAMA Mr. 2 a.k.a SUGU ANAPOAMUA KUGOMBEA UBUNGE!!!


Mwana-Harakati na Mkongwe wa Hip Hop Tanzania,Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu ametangaza nia yake ya kugombea Ubunge kwa tiketi ya CHADEMA, jimbo la Mbeya mjini.

Mheshimiwa mtarajiwa yuko Mkoani Mbeya akiwa kwenye mchakato wa kurudisha fomu baada ya kupata ridhaa ya chama chake...Mr. 2 au Sugu anaungana na wasanii wengine toka Tanzania kama Kalama Masoud a.k.a Kalapina anatakayegombea Udiwani jimbo la Kinondoni-DSM kupitia chama cha CUF na Nakaaya Sumary aliyetangaza nia ya kugombea Ubunge mkoani Arusha kwa tiketi ya CHADEMA... Daaaaaah!! huu ni mfano wa kuigwa kwa wasanii hawa wa muziki wa Hip Hop nchini.. Na ukisikiliza ngoma zao kwa makini utasikia wanazungumzia mambo ya kijamii indeep......! so waheshimiwa kila la kheri 2010.....    Sourcempangomzima.blogspot.com 

MB DOGG "REP YO COUNTRY" LONDON AFRO JAM EXPERIENCE SATURDAY 1OTH JULY.

MB DOGG LIVE "REP YO COUNTRY" LONDON AFRO JAM EXPERIENCE SATURDAY 10TH JULY


★•★•★•★•★•★BONGOUK REP YOUR COUNTRY BASH 2010•★•★•

•★•★•REP YOUR COUNTRY "LONDON AFRO JAM EXPERIENCE" FT MB DOGG• •★•★•★•★•★•★•★

•★•★•FOR THE FIRST TIME EVER MB DOGG LIVE IN THE 
UK TO RISE UP THE FIRE FOR THIS SUMMER WITH HIS BIGGEST HITS 

•★•★•★•★•★•★LATIFA•★•★•★•★•★•★

•★•★•★•★•★•★SI ULINIAMBIA•★•★•★•★•★•★

•★•★•★•★•★•★NAONA RAHA•★•★•★•★•★•★

•★•★•★•★•★•★MAPENZI KITU GANI•★•★•★•★•★•★

•★•★•★•★•★•★INA MAANA•★•★•★•★•★•★

•★•★•★•★•★•★SAGA PLASHER•★•★•★•★•★•★

•★•★•★•★•★•★PLUS MANY MORE•★•★•★•★•★•★

IS GOING TO BE A BANG COME REP YO COUNTRY AND BE PROUD OF OUR MUSIC


▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀
CLUB VALENTINO
750 TOTTENHAM HIGH ROAD
N17 0AL
LONDON

▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀▀

►FROM 
9PM TILL 5AM 

►ADM £15

►COME EARLY PARTY LONGER & AVOID DISAPPOINTMENT


►PROFESSIONAL PHOTO SHOOT

►TIGHT & POLITE SECURITY 

►BRING YOUR WHISTLES ! BRING YOUR VUVUZELA !

►WE GONN BRING THE ROOF DOWN