Thursday, May 6, 2010

NILIPOHUDHURIA MEDIA WORKSHOP YA CHAMPION..

Champion ni mradi unaotia hamasa na msukumo wa ushiriki wa wanaume ktk kujikinga na VVU ambao hupo chini ya shirika la EngenderHealth ukifadhiliwa na USAID. Jana nilipata nafasi ya kuwakilisha Ebony Fm ktk Moja ya Workshop iliyousisha vyombo vya habari na hasa wanahabari. ulifanyika Peacock Hotel jijini Dsm. Hapo juu ni mmoja wa watoa mada Sara Tesi alipokuwa akiwaelezea wanahabari jambo.
Mradi wa Champion unalenga kuhamasisha mjadala wa kitaifa kuhusu majukumu ya wanaumena kuongeza usawa wa kijinsia, hili kupunguza hatari ya wanaume,wanawake na watoto kupata VVU/UKIMWI. Hope unaniona ktk picha na wadau wengine tukifatilia kwa makini mtoa mada Dr. Ben...........
Hapo ni Dr. Ben Ngoye kutoka EngenderHealth akitoa Elimu juu ya HIV na pia akielezea jinsi gani Media inaweza kufanikisha kufikia malengo ya mradi huo katika jamii. (The Role of The Media).
Hapo ni wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakichangia mada juu ya nini kifanyike kati ya mradi na Media hili kutimiza malengo ya kufikisha ujumbe ktk jamii............
Wadau wakisikiliza kwa makini zaidi juu ya mpango mzima wa campaign za Champion kuhusu majukumu ya mwanaume na kuongeza usawa wa kijinsia.

Picha zote kwa hisani ya www.sufianimafoto.blogspot.com

No comments:

Post a Comment