Thursday, May 27, 2010

NDIVYO ALIVYOMALIZA BIZZO KATIKA MAKALA YAKE...


KIPINDI CHA PLANET BONGO EATV CHAPOTOSHA UMMA(Pt III)

              Katika mtiririko wa vipindi hivyo vya PLANET BONGO wasanii wa Arusha niliwasikia wakitetea hoja yao kuwa inawezekana MUZIKI huu ulianzia Arusha hata kabla ya Dar kwa kigezo cha kwenda Arusha kwa mwanaharakati nambari moja wa BONGO FLEVA Tanzania anayejulikana kama DJ JUMANNE bila kutaja mwaka ambao jamaa huyo alitia timu Bongo hii,ukweli ni huu,JUMANNE ndio aliyefanikisha safari ya kwanza ya SUGU barani Ulaya na utengenezwaji wa albam ya nne ya msanii huyo ya NJE YA BONGO ya mwaka 1999 baada ya NIITE MR II ya mwaka 1998,sasa hiyo inaonesha wazi kuwa kama JUMANNE aliwahi sana kwenda Arusha kama wasanii wa huko wanavyodai basi haikuwa kabla ya 1995,wakati ambao tayari MUZIKI Mwanza ulikwishaanza zamani sana,na nataka niwaambie kitu kimoja wasanii wa Arusha, kuwa JUMANNE alikwenda Arusha kwa sababu za kitalii zaidi na sio kwa kuwa Tanzania hii hakukuwa na MUZIKI eneo jingine lolote.Na awali kabisa alivutiwa na X-PLASTAZ ambao ndo BABA wa HipHop ya Arusha.Ishu ingine ni hii,mmoja kati ya mapromota wa kwanza kabisa wa MUZIKI huu Tanzania hii ni jamaa mmoja anaitwa RENA CALIST(Muandaaji Miss East Africa now),huyu jamaa ni mwenyeji wa MWANZA na suala la kuandaa matamasha alilianzia Mwanza kwa kuandaa matamasha ya “BINGWA WA RAP” Mkoa mwanzoni mwa miaka ya 1990 na baadaye mashindano kama WHOZ DA MAN yakaendelea.Kabla sijasahau MWANZA pia ni mkoa wa pili kuwa na redio station baada ya Dar(Radio Free Africa) ambayo ilianza mwaka 1995 mwishoni,kwahiyo ni moja kati ya vitu vikubwa vilivyochangia maendeleo ya muziki huu ambao tayari ulikuwepo.Shahidi mwingine ni aliyekuwa mtangazaji wa Radio One wakati huo ambaye aliacha kazi pale kwa harakati hizihizi za kuutambulisha muziki huu na kuhamia RFA mwaka 1996 TAJI LIUNDI(MASTER T),huyu alikuta MUZIKI uko tayari MWANZA na vijana wameaanza kurekodi japo kwa studio zilizokuwa chini ya kiwango.Nina mengi sana ya kuzungumza jamani juu ya utetezi wa point yangu kuwa si kweli kwamba Arusha ndio chimbuko na ndo kuna muziki zaidi ya Mwanza.
                Mwanza kuna kila kitu leo kinachoweza kuupeleka muziki mbele zaidi,Radio kubwa kuliko zote katika nchi za Maziwa Makuu iko Mwanza na pia ndio redio pekee yenye usikivu mkubwa Tanzania nzima(RADIO FREE AFRICA),TV station kubwa yenye wigo mpana TANZANIA pia iko Mwanza(STAR TV),watangazaji wanaoijua kazi na wenye hamasa na moyo wa kuutangaza muziki wa Mwanza pia wako kibao kule,hata hao wasanii wa Arusha wanaodai kuwa Arusha ndio kuna muziki zaidi kuliko Mwanza wanategemea promo kutoka kwa watangazaji na media hizo,sasa iweje leo Mwanza iwe chini??Kikubwa nnachoweza kuwashauri wasanii wa Mwanza wa leo,wasilewe na vijisifasifa wanavyovipata kwa airtime ndogo wanayoipata toka katika viredio vidogo vidogo vya hapo mjini,wajitume na watumie rasilimali iliyomo jijini humo kuufanya muziki wao uwe juu zaidi,washirikiane na wadau wa muziki jijini humo,waige mifano ya malegendari waliopita na wakubali ushauri toka kwetu sisi kaka zao,waache uadui usiokuwa na tija na watangazaji wa redio za hapo mjini,zaidi watengeneze NETWORK ili waweze kujitangaza kimataifa na sio kuridhika na tusifasifa wa kijinga.
               My last point but not list japo ninazo zingine nyingi,kama nilivyoeleza katika aya ya kwanza ya makala hii,kuwa kipindi ambacho kilirekodiwa Arusha si kipindi ambacho kilitengenezwa jana wala juzi,ni kipindi cha muda mrefu kidogo na kilitengenezwa na mtangazaji wa kipindi cha 5 CONNECT wakati EATV imeanza kuonekana Arusha na Moshi kama karibu kwa wakazi wa mikoa hiyo,hivyo nachelea kusema kuwa kipindi cha Arusha kilikuwa kimeandaliwa na kilifanyika kwa kutafuta wanaojua kuzungumza na MEDIA na wanaoujua MUZIKI wa Arusha vizuri tofauti na kipindi kilichotengenezwa Mwanza.Nadhani ndio maana Arusha ilionekana kuna MUZIKI zaidi kuliko Mwanza kitu ambacho nina uhakika si kweli.Jamani haya ni mawazo yangu tu mimi binafsi na wala yasimkwaze yeyote atakayesoma makala haya,ila naomba watangazaji na waandaaji wa vipindi mbalimbali vya redio na Tv wafanye tafiti za kutosha kabla na baada ya kutengeneza vipindi vyao na kabla ya kuvipeleka hewani,hii itapunguza kama si kuondosha kabisa mkangayiko na jamii kupelekewa taarifa zisizo sahihi juu ya mambo mbalimbali.Akhsante kwa kusoma mwanzo mpaka mwisho makala haya na kama una mchango,maoni au ushauri basi wasiliana nami kwa email zifuatazo bizzo4shizzo@ymail.com au renatuskiluvia@ymail.com

            ...................................MWISHO..........................

No comments:

Post a Comment