Tuesday, May 11, 2010

HONGERA KAKA MARTIN KWA KUMPATA WA UBAVU.

Kila jambo jema ni shukrani kwa Mungu, akiwa na uso wa furaha iliyopitiliza kwenye siku aliyokua anaota ifike kwa muda wote wa maisha yake... ni Martin Mauya alipokimbia ukapela kwa kufunga ndoa tarehe 8/05/2010. Me pia nilikua mmoja ya waalikwa pale... Tukala bata mwanzo mwisho...
Hapo ni maharusi walipokalishwa mbele tayari kwa kupokea zawadi, na mtu mzima nikapata pix ya faster kama unavyomchek Bro Martin Deghe Mauya na bibie Magreth , huku wakiwa na nyuso za furaha sana. Nawatamania jamani...
Hapo sijui ni kamati gani au Bungeni nini? mcheki kaka Junken Milli ,Denis Soka na Samson Tibba a.k.a The General..... leo ni kama ilikuwa tofauti na siku nyingine wakati tukiwa tunapiga mzigo wa Tupo Pamoja.
Hapo kati anaitwa Annastazia Mairi but ufahamika sana kama Sada kama wewe ni mpenzi wa Tasnia ya filamu na maigizo hapa Bongo hope utakua unamsoma...... Nway ni mtangazaji wa show ya Jambo Rafiki hapa Ttv.. Some time anapiga  show moja matata ya Gospel inayoitwa Sauti Zetu Special hapa hapa Ttv..... Upenda sana kuniita Pompipoooooo cjui anamanisha nini huyu mdada?
Si ndio time ya kutoa zawadi kwa maharusi kutoka kwa wafanyakazi wenzake wa Ttv ikafika!!.. kwa pamoja tukawakilisha wachache ambao hawakufika kutokana na majukumu mbalimbali.... Hawa madada matata, mmoja kutupia cha black mwingine cha Red walipendeza sana bana........
Sasa, sasa, sasa bana ikafika muda wa lisebene mtu  mzima si nikavutwa na wadada nikacheze........... Eti oooh! we Pompipoooooo!! huwezi cheza sebene kama vipi ebu njoo..... mbona ilikuwa balaaaa!!!!....... Flower iliyopigia kitu cha White anaitwa Frida na mbele yake mwenye maua ua ni Messe Meena mwadada wa Dodoso la wiki Ttv.
Kama watu wote hawakuamini kilichotokea pale, wakajiuliza huyu ndio Arnie Gizzle wa Tupo Pamoja???????? Kushtuka mtu mzima nipo kati nabanjuka na Anna  flower wa Jambo Rafiki.... Daaaah ilikuwa balaaaaaa!! ........Maji ufuata mkondo wake mwenye viatu red ni Aneth Nyoni, mdogo wake na Ruiza Mbutu wa Twanga!! Mmmmmh ni noma kwa sebene!!!!!!!!
Mwisho wa siku tukashow some Love kwa maharusi kwa pix za hapa na pale.... hizo black suit utazani watoto wa White House kumbe watoto wa Baba Askofu pale Tumaini Tv...... Bro Martin , kwa niaba ya wafanyakzi wote wa Radio/Tv Tumaini nakutakia maisha mema ya furaha kipindi chote cha maisha yako na familia yako. Mungu akutangulie na akusimamie........ ALL THE BEST!!!!!!!!!!! 

No comments:

Post a Comment