Thursday, April 22, 2010

NGURUWE PART II. IPO KITAA

Mamba Dudu Baya kweli ni Dudu tena Dudu mla watu, Nguruwe Project part 11 sasa ipo mtaan na mdau nimedondoshewa jana asubuhi ofisin kwangu, pia nikaituma Iringa pale Ebony Fm kwa mwanangu (mfanyakazi mwenzangu) mnyamwezi Eddo wa The splash show hili awashibishe wadau na wanaharakati wenzetu ambao sio manguruwe

Humo ndani kunatisha, Kawachana live bila chenga mameneja wa wasanii hasa pale alipogusia kuhusiana na suala labaadhi ya wasanii waliokua TIP TOP Connection walivyozimwa kama taa hasa MB Dog na Albamu ya Latifah, Pia waliozimwa kabisa kama taa ni Z-Anto, Spark, Pingu na Desso..............................

Hakuishia hapo, zaidi aliponda show fake za bongo, zinazoandaliwa na baadhi ya Radio zinazowakumbatia manguruwe ....... Na kwa msisitizo katumia mstari uliyopo kwenye ngoma ya stimu zimelipiwa ya Mwamba wa kaskazini JOH Makini unaosema DAI PESA, UZIMWE KAMA TAA........................
Mbaya zaidi ni pale alipomfananisha Ney wa mitego kama mwanamke Malaya aneongwa gari bila kadi yake..... Hapo Dudu anasema manguruwe walimtumia Ney kama mamuluki kuwasagia wasanii ikiwa ni moja ya mikakati ya manguruwe hao kuwakandamiza wanaharakati waukweli kama P-Funky Majani hili wawanyanyue wakwao.........Lakini baada ya ngoma yake kupewa promo ya kutosha kwa maslahi yao (manguruwe) wakampiga Ney kibuti, akaongeza kwa kusema Ney ana zaidi ya ngoma mpya 3 lakini no AIR............

Dudu kazungumza mengi na kwa upana zaidi.... Naweza jaza ukurasa ,so fanya kuitafuta part 11 au sikiliza baadhi ya Radio wanaiendeleza...... kwenye hiyo Revolution nipo nyuma yako DUDU THE MAMBA!!!!!!!!!!!!!

ZAIDI WATCH 2PO PA1 SHOW KESHO SAA 3 usiku ON Ttv

4 comments:

 1. Hey kaka inakua vipi kama ukiweka katika blog yako hii ishu ili tujue ni nini kimeongelewa humo maana wengine tupo mbali na home.

  ReplyDelete
 2. mie naungana na dudu kua manguruwe wako wengi nakukumbusha kitu kimoja unakumbuka wakati mr blue na ngwear walivyokua chini ya zizzou fashen baada ya kutoka kwa zizu wamezimwa kama taa coz watangazajina na madj walikua wanapata chochote wakitembelea kwa zizu ila sasa huwasikii tena hao wasanii yaani wametupwa kulee naamini asemayo dudu ni ukweli mtupu ila ukitaka kuonekana mbaya useme ukweli hasa kwa nchi hii tena kama watu wanaweza kukutengenezea kesi ili wakupteze kabisa wakutengenezea wasnii jitokezeni ktk hili coz ni haki yenu ninyi na media mnategemeana ni mawazo tu msijenge chuki wazee ni mkurya halisi tika musoma

  ReplyDelete
 3. mie naungana na dudu kua manguruwe wako wengi nakukumbusha kitu kimoja unakumbuka wakati mr blue na ngwear walivyokua chini ya zizzou fashen baada ya kutoka kwa zizu wamezimwa kama taa coz watangazajina na madj walikua wanapata chochote wakitembelea kwa zizu ila sasa huwasikii tena hao wasanii yaani wametupwa kulee naamini asemayo dudu ni ukweli mtupu ila ukitaka kuonekana mbaya useme ukweli hasa kwa nchi hii tena kama watu wanaweza kukutengenezea kesi ili wakupteze kabisa wakutengenezea wasnii jitokezeni ktk hili coz ni haki yenu ninyi na media mnategemeana ni mawazo tu msijenge chuki wazee ni mkurya halisi tika musoma

  ReplyDelete
 4. Daaah..... am so sad coz nimekikosa kpndi chako, kwani kinarudiwa lini? kama vp weka bana hiyo issue ya manguruwe kwenye blog yako itakuwa mbalatata zaid!

  ReplyDelete