Saturday, October 11, 2014

KANDA YA ZIWA - TOUR TO GEITA.


Journey ilianza majira ya saa `10 alfajiri.. kutoka Dar es salaam kupitia Moro, Dom, Singida, Nzega-Tabora, Shinyanga, Mwanza mpk Destination yetu Geita. Nikiwa na my Young Bro Fredy.. Geita ni moja kati ya mikoa mipya nchini. sifa kubwa ya mkoa huo ni migodi ya Dhahabu , kuanzia wachimbaji wadogo mpk mgodi mkubwa wa GGM (Geita Gold Minning).....


Safari haikua mbaya sana japo kukutana na changamoto za hapa na pale.. kabla ya kufika Nzenga tulipata BreakDown ... hvyo tulipark ili kubadilisha Tyre..... All in all namshukuru Mungu tulifika salama.

Nilipata chance ya kutembelea moja ya migodi ya wachimbaji wadogo ambao unamilikiwa na mmoja ya wanafamilia.... Dhumuni ilikua ni kujifunza jinsi ya uchimbaji wa madini aina ya Dhahabu na hatua zinazopitiwa mpk kuingia sokoni tayari kuuzwa..

Magunia hapo juu ni mawe ambayo yana dhahabu yakiwa tayari kwa kusagwa!!

Hapa ni moja ya wafanyakazi akiwa ktk hatua ya mwisho ya kuosha kwa Mercury then kuchomwa moto kuwa dhahabu......Ni moja kati ya wafanyakazi wa mgodi wakiwa wanaponda mawe tayari kwa kusangwa kwa mashine then kuoshwa kwa hatua ya kwanza kama inavyoonekana hapo chini.


Me pia nikapata time ya kushiriki na wadau kama kawaida yangu ku-share na wenyeji na pia kujifunza kutoka kwao.... Hapo wakinionyesha jinsi ya kuosha na pia hatua moja baada ya nyingine.. Lakini pia tuliongea mengi ikiwamo na changamoto wanazokabiliana nazo... kubwa ikiwa ni usalama wao kazini na viotendea kazi Duni!!!


Haya jembe piga kazi tuone tunalijengaje Taifa Letu!!
Hatua ya tatu toka mwisho ni kuosha yale machujio ili kutoa particle zilizobakia humo ndani.. Anyway was fun to me kufanya kazi na wenyeji wangu!!!Haya ni mazingira ambayo yapo jirani na mgodi huo ... lakini kwa upande mwingine ni vyanzo vya maji kitu ambacho ni hatarishi kwa mazingira kutokana shughuli zinazoendelea mgodini hapo.
Then nikapata chance ya kutembelea vyanzo hivyo vya maji. Mazingira bado ni mazuri na yanavutia maana bado ya uhalisia wake.


Hapo juu ni mfanyabiashara wa mawe yanayosadikiwa kuwa na dhahabu ambayo huyauza kwa wachimbaji wadogo wadogo na baadae utaratibu wa kuyasaga unafuata!!...

Baada ya hapo nikapata Ziara ya kutembelea shamba kubwa la mahindi na mihogo nje kidogo na mji wa geita. Pia nilipata kujifunza mengi kuhusu kilimo na faida zake...
 

Siku iliyofuata nikatembelea shamba lingine la vitalu vya miche mbalimbali ya miti na maua. (Nursery)... likini pia ufugaji wa wanyama na kuku...


Safari yangu kwa ujumla ilikua nzuri maana nilijifunza mengi  sana!! kwa manufaa yangu na nchi yangu Tanzania.....!!!!!!!

Ziwa Victoria ni ziwa kubwa kuliko yote barani Afrika, na la pili Duniani.  Huku Ziwa la kwanza kwa ukubwa Duniani ni Ziwa Superior ambalo lipo North America.Hivyo kama watanzania tuna budi kujivunia Ziwa letu ambalo lina eneo la kilometa za mraba zaidi ya 68,100 huku maji yake yanamiminika kwenye mto Nile na kuelekea Bahari ya Mediteranea kwa umbali wa maili 4,000.


Ziwa Victoria ni kitega uchumi kikubwa kwa wakazi wa kanda ya Ziwa kama vile Mwanza, Mara, Kagera na mikoa jirani ikiwemo mkoa wa Geita wenyewe.... Lakini pia ni  kiunganisho na mpaka kwa nchi Majirani zetu wa Afrika Mashariki ambao ni Kenya na Uganda. Huku Tanzania tukiwa na Eneo kubwa la maji ukilinganisha na wenzetu Kenya na Uganda. Ambapo Tanzania tuna 49% ambazo ni sawa na 33,700 km2 huku tukifatiwa na Uganda ambao ni 45% sawa na 31,000 km2 na Kenya ikiwa na asilimia 6% sawa na 4,100 km2 ya eneo la ziwa.


Ziwa Victoria linapata maji yake mengi kutokana na mvua (80%) na asilimia chache kutoka vijito vingi vidogo. Mto mkubwa unaoingia ziwa Victoria ni Mto Kagera ambao unatiririka kutoka upande wa magharibi wa ziwa Victoria.

Ziwa Victoria lina kina cha wastani cha mita 40 sawa na futi 130, na mwambao wa urefu wa mita 4,828 sawa na maili 3,000, huku visiwa vyake vikiwa vimechangia 3.7% ya urefu huu.

Hii ni moja ya feri inayofanya safari zake kutoka upande mmoja wa Busisi kwenda upande mwingine.. nili-enjoy sn safari yangu maana niliona na kujifunza mengi .. Utalii wa ndani.... 

KEEP VISITING  4 MORE INFO..!!!


Wednesday, October 8, 2014

..........INSTAGRAM PARTY IN MWANZA.............FreconicIdeaz ndio walio-organize Instagram Party Event, ambayo ilifanyika tarehe 04/10/2014 pale kati Jembe ni Jembe a.k.a Jembe Beach iliyopo Rock City - Mwanza.

Usiku wa Party kulikua na Live Performances kutoka kwa wasanii wa Music wa kizazi kipya, dancing, kufamiana na pia kusalimiana kwa fans na followers kulihusika na mengine kibao.
Ben Pal na Songa ni moja kati ya wasanii waliofanya Live performances hapo wakiwa na Fan wao waki-show Love .

Instagram ni moja ya kati ya mitandao za kijamii ambayo uwapa fursa watumiaji wake ku-share information kupitia picha na Video, ni moja ya mitandao ya kijamii unaokua kwa haraka sana duniani na hapa kwetu Tanzania kutokana na urahisi wa upatikanaji wa Smart Phones.Party ilipendezeshwa na Ma-Dj's kama vile Dj Vasley na Dj Dommy huku ikiwa Hosted na Raheem Da Prince.
INSTAGRAM PARTY TZ inatokana na matokeo ya kuongezeka kwa watumiaji wa Instagram Tanzania. Instagram Party Tz ni platform ya kuburudishana, kufamiana na pia kufanya socialization kwa watumiaji wa instagram ikihusisha wanunuzi, wauzaji, mashabiki na public figures.

Instagram party TZ inahusisha series za matukio kutoka sehemu mbalimbali na kwa theme tofauti kama vile;- Instagram Barbeque Party, Instagram All starsParty,Instagram Beach Party,Instagram The LoungeExperience, Instagram First Fridays, InstagramBirthdays Bash etc.


Upcoming Instagram Parties ......  Kwa mikoa ya Dodoma na Mbeya tukutane terehe 25/10/2014 na pale kati Dar es salaam itakua ni tarehe 1/11/2014.


For More Information contact:
Check our Instagram page @instagrampartytz